Kucha (Hyliota)
(Elekezwa kutoka Hyliota)
Kucha | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Kucha wa jenasi Hyliota ni ndege wadogo ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba ndege hawa hawana mnasaba na Sylviidae. Labda wana mnasaba na familia Promeropidae (ndegesukari wa Afrika Kusini). Hadhi yao haijaamua bado lakini wapewa familia yao kwa sasa: Hyliotidae. Wanafanana na tatata. Kucha hawa wana rangi ya nyeusi au zambarau mgongoni na nyeupe, machungwa au njano chini. Hula wadudu na pengine beri na mbegu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito. Jike huyataga mayai 2-5.
Spishi za Afrika
hariri- Hyliota australis, Kucha wa Mashona (Southern Hyliota)
- Hyliota flavigaster, Kucha Tumbo-njano (Yellow-bellied Hyliota)
- Hyliota usambara, Kucha wa Usambara (Usambara Hyliota)
- Hyliota violacea, Kucha Mgongo-zambarau (Violet-backed Hyliota)