Ibn Battuta Mall ni duka kubwa lililoko katika barabara ya Sheikh Zayed mjini Dubai karibu na Interchange 6 ya kijiji cha Jebel Ali. Jina lake linatokana na msafiri maarufu Ibn Battuta. Mradi huu ulimalizwa na kampuni ya Nakheel mapema 2005. Majina ya maeneo sita ya duka hili yametokana na nchi ambazo Ibn Battuta alitembelea.

Ibn Battuta Mall
MahaliDubai,
Bendera ya Falme za Kiarabu United Arab Emirates
Tarehe ya ufunguzi2005
UongoziNakheel
MmilikiNakheel
Tovutiwww.IbnBattutaMall.com

Duka hili limegawanyika katika maeneo kuu sita:

  1. Uchina
  2. India
  3. Uajemi
  4. Misri
  5. Tunisia
  6. Andalusia


Saa iliyo na muundo wa Tembo katika Ibn Battuta Mall.

Ikiunganisha maeneo ya ununuzi, maeneo yote makuu yanayopatikana katika karibu maduka yote Dubai na Mashariki ya Kati yanawakilishwa. Géant, supamaketi kubwa ya Kifaransa duka hapa. Duka hili ni mfano wa moja ya miradi ya Nakheel katika Dubai.

Duka kubwa la rejareja la Australia la Myer limetangaza kuwa litakuwa na duka lililokamilika mwaka 2010.

Ibn Battuta inaringa kwa kuwa na sinema ya IMAX ya pekee nchini na pia iko na sinema ya skrini 21 katika eneo la Uchina. Kuna maeneo mawili makubwa ya chakula, yaliyoko katika miisho yote miwili ya duka hilo (Maeneo ya Andalusia na Uchina), na pia iko na maduka kadhaa ya kahawa yaliyotawanyika kote.


Duka hili lina maonyesho ya mavumbuzi ya kitambo ya kiteknolojia, hususan kutoka Mashariki ya Kati. Hizi ni pamoja na saa iliyo na muundo wa tembo, uvumbuzi wa kiislamu ulio na saa inayopata nguvu kutoka kwa maji iliyo na muundo wa tembo.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons