Ilani ya Wanawake kwa Ghana

Ilani ya Wanawake ya Ghana ni kauli ya kisiasa ya wanawake wa Ghana wanaotaka haki na usawa. Ilitolewa mwaka 2004 na inaendelea kushawishi uandaaji wa wanawake kushiriki katika nyanja mablimbali kama siasa, uchumi na mambo ya kijamii kwa usawa nchini Ghana.

Historia ya Ilani ya Wanawake nchini Ghana hariri

Ilani hii ilitokana na kuongezeka kwa uandaaji wa wanawake nchini Ghana, hasa kuhusu mswada wa masuala ya unyanyasaji wa nyumbani na pia uchaguzi wa mwaka 2000. Maandalizi hayo pia yaliambatana na idadi kadhaa ya mauaji ya wanawake katika mji wa Accra, ambayo yalisababisha maandamano katika Ngome ya Osu. Wanaharakati pia walipinga uundwaji wa Wizara ya Masuala ya Wanawake, ambayo waliamini itashughulikia masuala ya wanawake nyumbani mwao.[1]

Kampeni ya uhamasishaji iliungwa mkono na NETRIGHT, mtandao wa haki za wanawake nchini Ghana na ABANTU for Development, asasi iliyoanzishwa na wanawake wa Kiafrika waishio na kufanya kazi barani Ulaya.[2] [3] Waandalizi walikataa kuungwa mkono na wafadhili ambao walitaka kubadilisha vigezo vya kampeni.[1]

Mkutano ulifanyika ili kuwakutanisha wanawake kutoka wilaya 110 zinazopatikana katika mikoa ya nchini Ghana, ili kuweza kugundua mfanano na tofauti katika masuala ya wanawake nchini kote. Mikutano hii ilizalisha orodha ndefu ya desturi za kitamaduni, kama vile ukosefu wa usawa katika ndoa na elimu, ambazo wengi wao walitaka kuzibadilisha. Waandalizi watatu walisema katika mahojiano yao kwamba walishangazwa na uwezo wa kundi kubwa kama hilo kuweza kufikia makubaliano juu ya malengo ya harakati za wanawake wakati wa kuandaa waraka huo.[1]

Yaliyomo hariri

Manifesto ilitaka ushiriki sawa wa wanawake katika mfumo wa uongozi wa serikali ya Ghana, ikitaka bunge liwe na 30% ya wawakilishi wanawake ifikapo mwaka 2008 na 50% ya wanawake ifikapo mwaka 2012.[4] Pia ilitaja ushiriki sawa wa wanawake katika uongozi wa vyama vya siasa nchini humo.[4][5] Ilani hiyo pia inaelezea hali ya kila siku ya wanawake nchini Ghana na inaelezea kwamba serikali lazima ichukue hatua kuhakikisha haki za wanawake zinasimamiswa ipasavyo ifikapo mwaka 2010.[5] Inaelezea kwamba serikali ihakikishe wanawake wanapata huduma salama ya afya ya uzazi, ikijumuisha na utoaji mimba.[4]

Ilani inatambua jukumu la ukosefu wa usawa wa kiuchumi na ugandamizwaji wa wanawake na watu maskini na inadai kipato cha chini kabisa kwa watu wote wa Ghana.[6][7] Ilani inaeleza mahitaji maalum na changamoto za wanawake wenye ulemavu ilivyo ngumu wao kupata rasilimali muhimu na kuongezeka kwa viwango vya unyanyasaji wa kijinsia.[8]

Uzinduzi Wake hariri

Ilani ya Wanawake nchini Ghana ilizinduliwa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Accra tarehe 2 Septemba 2004. Waraka huu ulitangazwa sana na kupata umaarufu mkubwa licha ya serikali kutoa sera ya jinsia kwa kipindi cha nyuma.[1] Wazo kuu la ilani hiyo ilitaka kujua na kutatua matatizo yaliyokuwa yanawaathiri wanawake.

Matokeo hariri

Kundi lililounda ilani hiyo lilijiita Muungano wa Ilani ya Wanawake. Kikundi hicho bado kinasalia kikifanya kazi katika kukuza haki za wanawake nchini Ghana.[9] Tangu kuundwa kwa Ilani hiyo mwaka wa 2004, serikali ya Ghana imepitisha Sheria kuhusu Unyanyasaji wa Majumbani, Sheria ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Sheria ya Ulemavu, na imepiga marufuku vitendo vya ukeketaji wa wanawake.[10] Kundi hilo, pamoja na NETRIGHT, walifanya maandamano mwaka wa 2007 kupinga kutengwa kwa wanawake katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Ghana.[11]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Redirect". cdn.itskiddoan.club. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-07. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-03. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  4. 4.0 4.1 4.2 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-26. Iliwekwa mnamo 2022-03-31. 
  5. 5.0 5.1 "Women's Manifesto celebrates one year in Ghana". GhanaWeb (kwa Kiingereza). -001-11-30T00:00:00+00:00. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.  Check date values in: |date= (help)
  6. https://www.socialwatch.org/node/11024
  7. Manifesto (2004), p. 23: "Other elements of social development include food security, social security (such as pensions), housing and economic services such as transport infrastructure. In any case, a more comprehensive approach to social policy and social development must also include access to a minimum level of income for all citizens of working age and all families. In Ghana and elsewhere, the ability to earn an income is the defining feature of each individual. Those who are unable to do so find themselves at an enormous disadvantage and have some of the lowest status in society. As the majority of people in this situation are women, no comprehensive, progressive social programme can exclude the provision of minimum levels of income for all citizens and for women in particular."
  8. Nepveux, Denise M. (2006-09-15). "Reclaiming Agency, Ensuring Survival: Disabled Urban Ghanaian Women's Negotiations of Church and Family Belonging". Disability Studies Quarterly (kwa Kiingereza) 26 (4). ISSN 2159-8371. doi:10.18061/dsq.v26i4.814. 
  9. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/artikel.php?ID=89449
  10. http://pathwaysghana.blogspot.com/2009/09/five-years-after-womens-manifesto.html
  11. https://muse.jhu.edu/article/241433

Viungo vya nje hariri