Ilolangulu (Mbogwe)
Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa
Ilolangulu ni moja kati ya kata zinazounda halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,703 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 30414.
Kata hii inaundwa na vijiji 4 na wakazi wa eneo hili ni hasa wa makabila ya Wasumbwa, Wasukuma na Waha na ndiyo kata aliyozaliwa mbunge wa jimbo la Mbogwe, Augustine Manyanda Masele.
Wakazi wa kata hii ni wakarimu na wanajihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji. Wanalima nyanya, pamba, tikiti na mahindi.
Marejeo hariri
Kata za Wilaya ya Mbogwe - Mkoa wa Geita - Tanzania | ||
---|---|---|
Bukandwe | Bunigonzi | Ikobe | Ikunguigazi | Ilolangulu | Iponya | Isebya | Lugunga | Lulembela | Masumbwe | Mbogwe | Nanda | Ngemo | Nhomolwa | Nyakafulu | Nyasato | Ushirika |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |