Insha ya kisanaa
Insha ya kisanaa ni insha inayotumia lugha ya kisanaa, yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tasifida, tashbiha, tashihisi, tabaini, balagaha.
Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, ritifaa na tanakalisauti.
Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto kama nahau, methali na hizo tamathali za semi.
Sifa za insha za kisanaa
hariri1. Huwa na uteuzi wa maneno: insha za kisanaa hutumia maneno maalumu ya kisanaa na yanayovutia.
2. Huwa na lugha ya kisanaa: insha za kisanaa hutumia lugha ya kifasihi. Maneno ya kawaida hubadilishwa na kuwa maneno ya kisanaa; kwa mfano: "Njiwa yule ni mzuri". Sentensi hii ina maana kwamba mwanamke yule ni mzuri.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Insha ya kisanaa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |