Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia.

Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake.

Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani analoliunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo.

Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe kwa mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo insha anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo.

Mtiririko wa insha za hoja

hariri

Katika kuandika insha ya hoja, wafaa ufuate mtiririko huu:

  1. Anza kwa mvuto mkuu utakaomfanya msomaji apate uchu wa kuendelea kusoma. Huenda ukaanza kwa msemo uliosemwa na mtu fulani anayejulikana na wengi. Waweza pia kutaja takwimu kutokana na utafiti fulani uliofanywa. Waweza pia kuanza kwa hadithi fupi ya jambo lililokutokea na lina uhusiano mkubwa na hoja ambazo utazielezea.
  2. Baada ya mvuto huu mkubwa uliomteka msomaji, endelea kwa kumpa historia ya hoja yako. Historia hii humfanya msomaji aone kwamba hoja yako ina mizizi na kwa hiyo hujachukulia utafiti wako kijuujuu, bali umeufanya kwa kina.
  3. Toa hoja yako kwa kina na ukamilifu. Madhumuni ya insha yako ni kuitoa hoja kwa hali itakayoeleweka. Hakikisha kwamba umeitoa hoja vizuri kwa lugha nyepesi atakayoielewa msomaji
  4. Weka nukuu katika kazi yako. Baada ya kufanya haya yote, ni muhimu kunukuu maandishi mengine ambayo umetumia ili kuandika insha yako. Usipofanya hivi, itaonekana kana kwamba wewe ni mwizi wa hoja za wengine. Mtandaoni inapatikana misaada ya kutia nukuu katika kazi yako.

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Insha za hoja kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.