Ipasi wa Bitinia (kwa Kigiriki: ‘Υπατος Hypatos; 366 - 446) alikuwa mkaapweke mwenye kujinyima na kufunga sana kisha kukataa maelekezo ya baba yake mwanafasihi, labda kutoka Frigia, na kushika maisha magumu ya kitawa.

Halafu akawa abati wa monasteri aliyoijenga upya huko Kalsedonia, leo nchini Uturuki, ambapo alilea wafuasi wake katika nidhamu kamili ya kimonaki na walei katika uchaji wa Mungu.

Alipinga mafundisho ya patriarki Nestori.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu[1].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 17 Juni[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.