Iwambi
Iwambi ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Kata ya Iwambi | |
Mahali pa Iwambi katika Tanzania |
|
Majiranukta: 8°53′24″S 33°25′48″E / 8.89000°S 33.43000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mbeya |
Wilaya | Mbeya Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 9,181 |
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,387 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53115.
Iwambi iko kati ya Iyunga na Mbalizi kando la barabara kuu inayoelekea Vwawa na Zambia.
Iwambi ni kata ambayo kihistoria walipatikana kabila la Wasafwa ambao waliongea lugha yao ya Kisafwa pia waliongozwa na mwene Mpoli ambaye alifariki mwaka 2005 na alizikwa ndani ya Iwambi katika mtaa wa Ivwanga.
Kati ya wenyeji mashuhuri wa Iwambi ni John Butler Walden (1939 – 2002) aliyekuwa kiongozi mmojawapo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakati wa Vita vya Kagera dhidi Uganda. Kaburi lake linapatikana Iwambi. katika kata ya iwambi kuna shule mbili za msingi ambazo ni shule ya msingi iwambi ipo katika mtaa wa mayombo na shule ya msingi iyunga ipo katika mtaa wa Isoko pia wanashule moja ya sekondari Iwambi iliyo anzishwa mwaka 2006 chini ya uongozi wa raisi Jakaya mrisho Kikwete mbunge alikuwa ndugu [mpesya]] na diwani alikuwa MAJIGE hawa ndio viongozi waliosaidiA ujenzi huo wa shule ya sekondari iwambi kufanikiwa kusimama nakufanya vizuri katika mkoa wa Mbeya.
Marejeo Edit
- ↑ Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya MC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-14.
Kata za Jiji la Mbeya - Tanzania | ||
---|---|---|
Foresti • Ghana • Iduda • Iganjo • Iganzo • Igawilo • Ilemi • Ilomba • Isanga • Isyesye • Itagano • Itende • Itezi • Itiji • Iwambi • Iyela • Iyunga • Iziwa • Kalobe • Maanga • Mabatini • Maendeleo • Majengo • Mbalizi Road • Mwakibete • Mwansekwa • Mwansanga • Nonde • Nsalaga • Nsoho • Nzovwe • Ruanda (Mbeya) • Sinde • Sisimba • Tembela • Uyole |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Iwambi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |