Tuva (kwa Kirusi: Тыва) ni jina la jamhuri mojawapo ndani ya Shirikisho la Urusi. Iko katika Siberia ya kusini, kwenye kitovu cha kijiografia cha Asia.

Sehemu ya mkoa wa Tuva
Mahali pa Tuva katika Urusi

Imepakana na nchi ya Mongolia upande wa kusini na maeneo yafuatayo ya Shirikisho la Urusi: Jamhuri ya Altai, Jamhuri ya Khakassia, mikoa ya Krasnoyarsk Krai, Irkutsk Oblast na Jamhuri ya Buryatia.

Mji mkuu wake ni Kyzyl.

Idadi ya wakazi ni 307,930 (sensa ya mwaka 2010).

Kuanzia 1921 hadi 1944 Tuva ilikuwa nchi huru ya kujitegemea iliyojulikana kwa jina la Tannu Tuva. Mwaka 1944 iliingizwa katika Umoja wa Kisoveti na kuwa sehemu ya Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi, na baada ya anguko la Ukomunisti sehemu ya Shirikisho la Urusi.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tuva kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.