Jangwa la Chalbi ni jangwa dogo kaskazini mwa Kenya, kusini kwa mpaka wa Ethiopia.

Mandhari ya jangwa la Chalbi.

Liko mashariki kwa Ziwa Turkana ambalo ni ziwa kubwa kuliko yote duniani linalodumu ndani ya jangwa.

Mji wa North Horr umo katika jangwa hili. Mji mkubwa wa karibu ni Marsabit.

Jina la Chalbi limetoka katika lugha ya Wagabbra likimaanisha 'tupu'. Ni eneo lenye joto kubwa na yabisi katika Kenya.

Wenyeji wanaoishi kando yake na kuivuka ni Warendille na Wagabbra wanaotumia ngamia kwa usafiri.

Umbo la jangwa hili ni tambarare kabisa. Inaaminiwa ya kwamba miaka 10,000 iliyopita ilikuwa ziwa kubwa. Dalili zake ni visukuku vya kijiwe vya samaki na konokono vinavyopatikana huko.

Wakati wa mvua sehemu za jangwa zinafunikwa tena na maji kama ziwa lisilo na kina kirefu lakini hali hiyo haidumu.

Viungo vya nje

hariri

03°01′54″N 37°20′51″E / 3.03167°N 37.34750°E / 3.03167; 37.34750