Jeradi wa Beziers, C.R.S.A. (kwa Kifaransa: Guiraud; Puissalicon, Ufaransa, 1070 - Beziers, Ufaransa, 5 Novemba 1123) alikuwa kanoni, halafu priori, wa Waaugustino huko Cassan[1] .

Sanamu yake huko Beziers.

Mwenye uadilifu na unyofu mkubwa, mwaka 1121 alichaguliwa kuwa askofu wa Beziers[2] ingawa hakupenda, akazidi kufuata unyenyekevu katika cheo hicho kikubwa hadi kifo chake [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Novemba[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "CHATEAU-ABBAYE DE CASSAN Monument historique Histoire et patrimoine du Languedoc Roussillon". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-09. Iliwekwa mnamo 2024-10-14.
  2. Étienne Sabatier, Histoire de la ville et des évêques de Beziers (1854), p. 192.
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/76235
  4. http://pagesperso-orange.fr/ansart/Sanctoral/Annee/1105.htm, in French, under Saint Geraud, celebrated November 5.
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.