Jiminyano wa Modena

Jiminyano wa Modena (Cognento, Modena, Emilia-Romagna, Italia, 15 Januari 312 - Modena, 31 Januari 397) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 342/344 ingawa kwanza alikimbia jukumu hilo alipochaguliwa akiwa bado shemasi tu[1].

Mt. Jiminyano, alivyochorwa na Simone Martini, Fitzwilliam Museum, Cambridge.

Alimaliza Upagani jimboni na kupambana na Uario akishirikiana na Ambrosi wa Milano na alipata umaarufu kwa kufukuza pepo hata akaitwa Konstantinopoli akaponye binti kaisari.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Januari[2].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/39175
  2. Martyrologium Romanum, 2004
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.