Jina takatifu la Maria

Jina takatifu la Maria ni kumbukumbu ya hiari katika kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini. Huadhimishwa tarehe 12 Septemba kila mwaka[1] ili kuhimiza Wakristo kumsifu Bikira Maria na kumuitia katika shida yoyote.

Bibi Yetu wa Mawaridi alivyochorwa na William-Adolphe Bouguereau (1825-1905).

Historia ya adhimisho hariri

Adhimisho liliingizwa na Papa Innocent XI mwaka 1684, kufuatana na ushindi wa Wakristo dhidi ya Waturuki Waislamu katika Mapigano ya Vienna (1683).[2]

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano iliondolewa, lakini ilirudishwa tena na Papa Yohane Paulo II mwaka 2002, pamoja na kumbukumbu ya Jina takatifu la Yesu.

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. Ann Ball, 2003 Encyclopedia of Catholic Devotions and Practices ISBN 0-87973-910-X page 242

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jina takatifu la Maria kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.