João Lourenço
João Manuel Gonçalves Lourenço (amezaliwa 5 Machi 1954) ni mwanasiasa wa Angola ambaye ameshika nafasi ya Rais wa Angola tangu tarehe 26 Septemba 2017.
| |
Tarehe ya kuzaliwa | 5 Machi 1954 |
Alingia ofisini | 26 Septemba 2017 |
Kazi | Mwanasiyasa |
Hapo awali, alikuwa Waziri wa Ulinzi kutoka mwaka 2014 hadi 2017. Mnamo Septemba 2018 alikua Mwenyekiti wa Harakati za watu kwa Ukombozi wa Angola (MPLA), chama tawala. Alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kutoka mwaka 1998 hadi 2003.
João Lourenço aliteuliwa mnamo Desemba 2016 kuchukua nafasi ya nambari 1 ya chama katika uchaguzi wa wabunge wa Agosti 2017. Kwa upande wa katiba ya mwaka 2010, mtu anayeongoza orodha ya kitaifa ya chama cha siasa au umoja wa vyama vya siasa ambao hupata kura nyingi katika uchaguzi mkuu... atakuwa amechaguliwa Rais wa Jamhuri na Mkuu wa Utendaji (Kifungu cha 109). Kama MPLA ilishinda viti vingi 150, Lourenço moja kwa moja alikuwa Rais wa Angola, na kumpokea José Eduardo dos Santos, madarakani kwa miaka 38. Lourenço aliapishwa rasmi katika ofisi tarehe 26 Septemba 2017.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu João Lourenço kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |