John Korir
John Cheruiyot Korir (alizaliwa Disemba13, 1981) ni mwanariadha wa Kenya ambaye hujishughulisha na mbio za masafa Marefu. Anajulikana kwa sifa yake ya kungara katika majaribio lakini kushindwa katika mashindano makubwa[1].
Historia
haririKorir alizaliwa katika mji wa Kiramwok, Wilaya ya Bomet nchini Kenya. alianza kukimbia akiwa katika shule ya Msingi. Alifuzu kutoka Shule ya Sekondari ya Merigi mnamo 1998. Hatimaye alisajiliwa na Kikosi cha Kenya Army mnamo 2001. Yeye ni wa kabila la Kipsigis, ambalo ni tabaka dogo la Kalenjin.
John Cheruiyot Kori na John Kipsang Korir
haririJohn Cheruiyot Korir anafaa kutofautishwa kutoka kwa John Kipsang Korir ambaye sana sana hushiriki katika mashindano ya Amerika. Wawili hawa wameshindana mara kadhaa. Katika mashindano ya Lisbon Half Marathon ya 2002, Kipsang Korir aliibuka bora, huku Cheruiyot akimshinda Kipsang katika shindano la Cross Country nchini Kenya mnamo 2003.
Katika shindano la Cherry Blossom 10-Mile Run la 2005, John Cheruiyot Korir aliibuka wa tano katika huku John Kipsang Korir akilishinda shindano hilo[2][3].
Meneja na Kocha
haririMeneja wake ni Gianni Demadonna, huku kocha wake akiwa Renato Canova.
Mafanikio
haririMatokeo ya Kujivunia
haririUwanjani
- Mita 3000 7:43.35 (2000)
- Mita 5000 13:09.58 (2000)
- Mita 10,000 26:52.87 (2002)
Barabarani
- Kilomita 10 27:49 (2005)
- Kilomita 15 43:26 (2003)
- Half marathon 1:00:47 (2004)
Viungo vya Nje
hariri- IAAF wasifu wa John Cheruiyot Korir
- IAAF: Focus on athletes Ilihifadhiwa 2 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
Virejeleo
hariri- ↑ IAAF, 1 Desemba 2006 John Cheruiyot Korir, the favourite in Lagos - PREVIEW Ilihifadhiwa 5 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Cherry Blossom: 28 Machi 2005: Two John Korirs Meet; Sally Barsosio Favorite in Women's Race Ilihifadhiwa 17 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- ↑ "Cherry Blossom 10 Mile Road Race results 2005". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-17. Iliwekwa mnamo 2010-01-13.
- ↑ "Matokeo ya Addis Ababa 2008". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-03. Iliwekwa mnamo 2010-01-13.