John F. Kennedy
John Fitzgerald Kennedy (29 Mei 1917 – 22 Novemba 1963) alikuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1961 hadi alipouawa.
John F. Kennedy | |
John F. Kennedy mnamo Februari 1961 | |
Makamu wa Rais | Lyndon B. Johnson |
---|---|
mtangulizi | Dwight D. Eisenhower |
aliyemfuata | Lyndon B. Johnson |
tarehe ya kuzaliwa | Brookline, Massachusetts, U.S. | Mei 29, 1917
tarehe ya kufa | 22 Novemba 1963 (umri 46) Dallas, Texas, U.S. |
mahali pa kuzikiwa | Arlington National Cemetery |
chama | Democratic |
ndoa | Jacqueline Bouvier (m. 1953–present) |
watoto | Arabella Kennedy, Caroline Kennedy, John F. Kennedy Jr. na Patrick Bouvier Kennedy |
mhitimu wa | Harvard University |
Fani yake | Mwanasiasa |
signature |
Maisha
Alikuwa mtoto wa pili katika familia ya watoto 9. Baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu wa ukoo wenye asili ya Eire.
Vita Kuu ya Pili ilipoanza alijiunga na jeshi la wanamaji. Mwaka 1943 alijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na ndege za kivita za Japani.
Mwaka wa 1957 Kennedy alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu kwa ajili ya wasifu ya wabunge wanane wa Senati ya Marekani; kitabu kiliitwa Profiles in Courage.
Mwaka 1947 alianza kujiingiza katika siasa na mwaka 1960 alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Ni rais pekee muumini wa Kanisa Katoliki katika historia ya nchi hiyo.
Aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 22 Novemba 1963, akiacha mke na watoto wawili.
Atakumbukwa kwa kutetea haki za watu wote bila kujali rangi yao.
Kati ya mengine alisema "Wamarekani wasiulize Marekani imewatendea nini, bali wajiulize kwanza wao wenyewe wameitendea nini nchi yao".
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Maktaba ya John F. Kennedy tovuti rasmi
}}
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John F. Kennedy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |