0°14′58″S 42°37′51″E / 0.2495°S 42.6307°E / -0.2495; 42.6307Coordinates: 0°14′58″S 42°37′51″E / 0.2495°S 42.6307°E / -0.2495; 42.6307

Mto Juba
Daraja la mto Juba huko Baardhere (Bardera), Somalia
Chanzo Maungano ya mito ya Dawa na Gebele, Ethiopia
Mdomo Bahari ya Hindi kaskazini ya Kismayu
Nchi Ethiopia, Somalia
Urefu 1,659 km
Kimo cha chanzo ? m katika milima ya Bale, Ethiopia
Mkondo ? m³/s
Eneo la beseni 497,626 km²
Beseni la mto Jubba.
Mto Jubba karibu Jamaame.

Juba (pia: Jubba, Giuba, Ganane au Genale; kwa Kisomali Wabiga Jubba) ni mto mkubwa wa Somalia wenye maji mwaka wote. Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Ethiopia. Unaanzia karibu na mpaka wa Ethiopia, ambao Mto Dawa na mto Ganale Dorya inaungana, halafu unatiririkia kusini moja kwa moja hadi Bahari ya Hindi karibu na mji wa Kismayu, Somalia Kusini.

Wakati wa ukoloni mto Juba ulikuwa mpaka kati ya Kenya na eneo la Somalia lililokuwa chini ya Italia. Mwaka 1925 Uingereza iliwaachia Waitalia eneo la nchi kusini mwa mto (kwa Kiitalia: Territorio dell'Oltre Giuba - kwa Kiingereza: Jubaland).

Kila baada ya miaka kadhaa bonde la Juba huona mafuriko. Mafuriko mabaya yaliyoleta uharibifu mwingi yalitokea mwaka 1997.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Juba (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.