Juliani na Eunus (walifariki 251 hivi) walikuwa Wakristo wa Aleksandria (Misri).

Juliani, aliyekuwa hawezi kusimama kwa ugonjwa, alijitokeza kwa mahakimu akibebwa kitini na watumishi wake wawili. Mmojawao alikana imani, lakini Euno alidumu pamoja na mwajiri wake kumkiri Kristo.

Basi, walipandishwa juu ya ngamia na kutembezwa katika mji huo wote, halafu, kwa kupigwa hadharani kwa ajili ya imani yao, waliuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Habari zao, za askari Besas aliyejaribu kuwatetea na za wafiadini wengine kumi zimesimuliwa na barua ya Dionisi wa Aleksandria kwa Fabiani wa Antiokia.

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Februari[1] au 30 Oktoba[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.