Jumanne Mhero Ngoma

Jumanne Mhero Ngoma[1] (alizaliwa Makanya, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania[2], 1939) ni mtu ambaye serikali ya nchi ya Tanzania inasema aligundua madini ya Tanzanite.

Ugunduzi wa Tanzanite hariri

Katika mwaka 1967, alipokuwa na miaka ishirini na nane[2], Ngoma alikwenda Kiteto kutembelea familia yake. Aligundua madini ya buluu alipotembea nje. Akaleta madini haya katika basi mpaka Nairobi, Kenya – jiji ambalo lilitafiti madini zaidi ya Arusha, lakini watu wa Nairobi hawakuweza kugundua madini yake kilikuwa madini gani[3]. Baadaye, madini haya yalipelekwa Dodoma ili kuchunguzwa katika maabara. Hapa, Ian MacCloud (mtu ambaye anasoma jiolojia) alisema madini kile kilikuwa madini ya Zoisite[4]. Katika mwaka 1968, mwaka mmoja baada ya ugunduzi wa madini cha Tanzanite, duka la vito linaloitwa Tiffany & Co. lilianza kuuza madini hiki na lilikipa jina la “Tanzanite[5].

 
Tanzanite: Madini ambayo yaligunduliwa na Jumanne Mhero Ngoma.

Zaidi Kuhusu Tanzanite hariri

Watu ambao wanasoma madini wanafikiri kwamba madini cha Tanzanite yana thamani ya almasi kwa zaidi ya mara elfu moja. Yana thamani kubwa kwa sababu Tanzanite inapatikana katika nchi ya Tanzania tu – hakuna Tanzanite katika nchi yoyote nyingine[2]. Inapatikana ndani ya eneo la kilomita za mraba nane tu karibu na Mlima Kilimanjaro katika Eneo la Manyara. Pia, watu baadhi wanafikiri kwamba hakutakuwa na madini ya Tanzanite zaidi baada ya miaka kumi na tano kutoka sasa. Kwa hivyo, madini ya Tanzanite ni adimu sana[6].

Tuzo kwa Ugunduzi hariri

Miaka kumi na tatu baada ya ugunduzi wake, katika 1980, Mzee Ngoma alipewa cheti na shilingi elfu hamsini kutoka rais wa nchi ya Tanzania kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere[7]. Shilingi elfu hamsini ni sawa na kama dola ishirini na mbili leo[1]. Mzee Ngoma aliheshimiwa na rais Jakaya Kikwete pia katika mwaka 2015[4]. Miaka hamsini na moja baada ya kugundua Tanzanite, Mzee Ngoma alipata zawadi kubwa kwa ugunduzi wake. Tarehe sita, mwezi wa nne, mwaka 2018 elfu mbili kumi na nane, rais wa nchi ya Tanzania John Magufuli alimpa Mzee Ngoma shilingi milioni mia moja[7]. Pesa hii ni sawa na dola elfu arobaini na nne leo[2].

Tafsiri Tofauti ya Ugunduzi hariri

Mzee Ngoma alifariki tarehe thelathini, mwezi wa kwanza, mwaka 2019. Alikuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Dar es Salaam alipofariki[7]. Alikuwa na miaka themanini[2].

Jumanne Mgoma ni mtu ambaye serikali ya Tanzania inasema aliona madini cha Tanzanite kwanza. Lakini, watu wengine wanasema kwamba mtu wa kabila la Wamasai, Ali Juuyawatu, aligundua Tanzanite na alimuambia Manuel D’Souza, mtu ambaye anasoma kuhusu madini[6].

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 "Tanzanian gemstone finder living in poverty". www.aa.com.tr. Iliwekwa mnamo 2023-12-12. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Mweha Msemo (2019-02-03). "Face2Face Africa News - Face2Face Africa News %". Face2Face Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12. 
  3. "Govt moves to recognise Mzee Ngoma’s discovery of tanzanite". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-20. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12. 
  4. 4.0 4.1 "Tanzanite discovery hits 51th anniversary". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-13. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12. 
  5. The Tanzanite Experience. (2019, October). Discovery of Tanzanite. https://www.tanzaniteexperience.com/2019/10/
  6. 6.0 6.1 "A Rare and Beautiful Stone Fails to Shine: Tanzania’s Missed Opportunity". Knowledge at Wharton (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-12-12. 
  7. 7.0 7.1 7.2 "Tanzanite discoverer, Ngoma, dies at Muhimbili". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-08. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.