Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani

Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani (Kiing. Organization of the Petroleum Exporting Countries), kwa kifupi pia OPEC ni shirika la kimataifa linalounganisha nchi zinazozaa mafuta ya petroli. Makao makuu yako Vienna (Austria).

Nchi wanachama za OPEC

Kwa pamoja nchi hizi zina takriban asilimia 75 za akiba ya mafuta duniani katika ardhi yao. Kwa sasa zinalisha asilimia 40 ya mafuta yanayotolewa kila mwaka. Kutokana na kupungua kwa akiba za nchi zisizoshiriki katika OPEC inaonekana ya kwamba athira ya nchi za OPEC itakua.

Nchi wanachama

hariri

OPEC ina nchi wanachama 13 ambazo ni

  1. Algeria
  2. Angola
  3. Ecuador
  4. Indonesia
  5. Iran
  6. Iraq
  7. Kuwait
  8. Libya
  9. Nigeria
  10. Qatar
  11. Ufalme wa Uarabuni wa Saudia
  12. Falme za Kiarabu
  13. Venezuela

Kiini cha OPEC ni nchi za Waarabu.

Indonesia imetangaza ya kwamba inatarajia kuondoka katika OPEC kwa sababu mahitaji yake ya mafuta yanazidi kiasi cha mafuta inayozalisha.

Nchi muhimu zisizo wanachama

hariri

Kati ya nchi muhimu ambazo zinatoa mafuta mengi duniani kuna idadi ambazo si mwanachama kama vile Urusi, Marekani, China, Mexiko, Kanada, Norwei na Uingereza.

Shabaha

hariri

Nchi wanachama walijumuika kwa majukumu yafuatayo:

  • Kulinda shauku za pamoja za nchi zinazolisha mafuta ya petroli
  • Kujikinga dhidi mabadiliko ya bei ya mafuta ya petroli ya mara kwa mara
  • Kuhakikisha mblimbiko wa kutegemea kwa nchi wateja
  • Kuhakikisha ya kwamba nchi zinazolalisha mafuta yanapokea mapatoy a kutosha kwa mahitaji yao
  • Kuwa pamoja kuhusu siasa za mafuta

Mara nyingi OPEC haikufaulu kushikamana kwa nchi zote.

Kiasi cha mafuta kilichokubaliwa kwa kila mwanachama

hariri

Nchi wanachama zimepatana kati yao kiasi kwa kila nchi kinachotolewa na kuuzwa. Kipimo chake ni "mapipa kwa siku" na "pipa" moja ni swa na lita 158,98 za mafuta ya petroli. Kusudi la siasa hii ni nia ya kuzuia bei isishuke kwa sababu kama nchi moja inayohitaji hela inaanza kutoa mafuta mengi kumbe bei ya mafuta ingeshuka chini.

Kiasi kinachopasa kwa kila nchi ya OPEC na kiasi kinachozalishwa hali halisi kwa elfu za mapipa ya mafuta kwa kila siku (2007)[1]
Nchi Kiasi kinachokubaliwa (7/1/05) Uzalishaji (1/07) Uzalishaji unaowezekana
Algeria 894 1,360 1,430
Angola 1,900 1,700 1,700
Ekuador 520 500 500
Iran 4,110 3,700 3,750
Iraq 1,481
Kuwait 2,247 2,500 2,600
Libya 1,500 1,650 1,700
Nigeria 2,306 2,250 2,250
Qatar 726 810 850
Saudia 10,099 8,800 10,500
Falme za Kiarabu 2,444 2,500 2,600
Venezuela 3,225 2,340 2,450
Jumla 31,422 30,451 32,230

Viungo vya Nje

hariri
  1. Quotas as reported by the United States Department of Energy