Ekuador
Ekuador (kwa Kiswahili pia: Ekwado) ni nchi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini.
Ekuador |
---|
Jina la nchi kwa Kihispania (Ecuador) lamaanisha "ikweta", na sababu ni kwamba imekatwa nayo.
Imepakana na Kolombia, Peru na Bahari ya Pasifiki.
Funguvisiwa la Galapagos (Archipiélago de Colón) ni sehemu ya Ekuador ikiwa na umbali wa karibu kilomita 1,000 kutoka bara.
Watu hariri
Wananchi wengi (71%) wana mchanganyiko wa damu ya Kizungu na ya Kiindio. Wenye asili ya Afrika ni 7.2%, Waindio ni 7%, na Wazungu ni 6.1%.
Ekuador ilikuwa koloni la Hispania, hivyo lugha ya wakazi wengi na lugha rasmi imekuwa Kihispania hadi leo. Lakini kuna Waindio wengi, hasa katika milima ya Andes, wanaoendelea kutumia lugha zao.
Asilimia 91.95 wana dini, na kati yao 80.44% ni Wakatoliki ma 11.3% Waprotestanti.
Tazama pia hariri
Viungo vya nje hariri
- (Kihispania) Rais wa Ekuador tovuti rasmi Archived 6 Mei 2008 at the Wayback Machine.
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ekuador kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |