Just Stand Up!
"Just Stand Up!" ni wimbo ulioimbwa na mjumuisho wa wasanii mbalimbali, wanaoimba miondoko ya pop, R&B, rok, na Katri katika tamasha la kukusanya fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa saratani.Mtayarishaji na mtunzi wa nyimbo wa Marekani L.A Reaid aliandaa ushirikiano huo wa wasanii baada ya kukutana na mwanzilishi wa tamasha la Pingana na Saratanai, na kuandaa tamasha litakalosaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kukuza mfuko huo. Waandaaji hawa waliandaa wimbo huu, kwa kushirikiana na waimbaji wa Kimarekani kama vile Bebyface na single hii ilitoka tarehe 21 Agasti 2008
“Just Stand Up!” | ||
---|---|---|
Single ya Artists Stand Up To Cancer | ||
Imetolewa | Agosti 21, 2008 Septemba 30, 2008 (CD single) | (digital)|
Muundo | Digital download, CD single | |
Imerekodiwa | 2008 | |
Aina | Pop, R&B | |
Urefu | 3:34 | |
Mtunzi | Babyface, Ronnie Walton |
Waimbaji hawa waliimba wimbo huu moja kwa moja ambayo ilirushwa hewani katika vyombo vya habari mbalimbali kama vile ABC, CBS na NBC tarehe 5 Septemba 2008.[1][2] Single hii ilitolewa tena tarehe 30 septemba 2008, na pia ilitoka na nakala ya tamasha la moja kwa moja. Lakini single hii haikuwa na video yake.
Waimbaji
hariri- Mariah Carey
- Beyoncé Knowles
- Keyshia Cole
- Mary J. Blige
- Rihanna
- Carrie Underwood
- Fergie
- Sheryl Crow (only on studio version)
- Melissa Etheridge (only on studio version)
- Leona Lewis
- Natasha Bedingfield
- Miley Cyrus
- LeAnn Rimes (only on studio version)
- Ashanti
- Ciara
- Nicole Scherzinger (only on live version)
Onesho la moja kwa moja
haririOnesho la moja kwa moja, lilikuwa katika tamasha la Stand Up 2 Cancer lililofanyika tarehe 5 Septemba 2008, lililooneshwa katika vyombo vya habari mbalimbali. Waimbaji wengi walionekana ambao walirekodi wimbo huu isipokuwa, LeAnn Rimes, Sheryl Crow na Melissa Etheridge, na wapo walioongezeka kama vile Nicole Scherzinger kutoka katika kundi la Pussycat Dolls aliyeimba nafasi ya Sheryl Crow.
Orodha ya nyimbo
hariri- "Just Stand Up!"
- "Just Stand Up!" (Live Video)
Chati
haririWimbo huu uliingia katika chati ya Billboard Hot 100 katika wiki ya 78, ya tarehe 13 septemba. Wiki iliyofuatia ilifanikiwa katika mauzo na kuvuka nafasi takribani 67 na kufika hadi nafasi 11. Wiki iliyofuatia wimbo huu ulianguka na kushuka hadi nafasi na 36. Wimbo huu pia ulishaingia katika chati ya Uingereza na kufanikiwa kushika nafasi 39, na baadae kupanda hadi nafasi 26. Katika chati ya nchini Canada wimbo huu ulifanikiwa kufika hadi nafasi ya 10 katika wiki ya septemba 11.
Chati
haririChati (2008) | Ilipata nafasi |
---|---|
Australian ARIA Singles Chart[3] | 39 |
Austria[4] | 73 |
Canadian Hot 100[5] | 10 |
Italian FIMI Singles Chart | 7 |
Japan Hot 100 | 85 |
DSM Hot 25 Chart | 1 |
DSM Hot Pop Chart | 1 |
New Zealand RIANZ Singles Chart[6] | 19 |
Swedish Singles Chart[7] | 51 |
U.S. Billboard Hot 100[8] | 11 |
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs[9] | 57 |
U.S. Billboard Pop 100[10] | 18 |
UK Singles Chart | 26 |
Wafanyakazi
hariri- Kwa upande wa sauti – Carrie Underwood, Mariah Carey, Beyoncé Knowles, Mary J. Blige, Rihanna, Fergie, Sheryl Crow, Melissa Etheridge, Natasha Bedingfield, Miley Cyrus, Leona Lewis, Keyshia Cole, LeAnn Rimes, Ciara, Ashanti na Nicole Scherzinger (only on live version) Walishirikiana katika kutengeneza sauti.
- Beyoncé Knowles kutoka katika studio za Columbia Records.
- Mary J. Blige kutoka studio za Geffen Records.
- Rihanna kutoka studio za Def Jam Recordings.
- Fergie, Sheryl Crow kutoka A&M Records.
- Mariah Carey, Melissa Etheridge kutoka Island Records.
- Natasha Bedingfield kutoka Epic Records.
- Miley Cyrus kutoka katika studio za Hollywood Records.
- Leona Lewis kutoka katika studio za Sony BMG/Syco/J.
- Carrie Underwood kutoka Arista Nashville.
- Keyshia Cole kutoka Interscope-Geffen-A&M.
- LeAnn Rimes kutoka katika Asylum-Curb.
- Ashant kutoka Universal Records
- Ciara kutoka katika studio za Zomba Label Group, Sony BMG.
- Nicole Scherzinger kutoka studio za Polydor, A&M and Interscope (only on live version)
Marejeo
hariri- ↑ Kaufman, Gil. "Mariah Carey, Beyonce, Fergie, Miley Cyrus, More Collaborate On Cancer Benefit Single", MTV News, 2008-08-19. Retrieved on 2008-08-20. Archived from the original on 2010-12-24.
- ↑ Jessen, Monique. "Mariah Carey, Beyoncé Unite For Charity Record", People, 2008-08-20. Retrieved on 2008-08-26. Archived from the original on 2016-05-05.
- ↑ Just Stand Up! chart history - australian-charts.com. australian-charts.com. Retrieved on 28 Juni 2009.
- ↑ http://www.lescharts.com/showitem.asp?interpret=Stand+Up+To+Cancer&titel=Just+Stand+Up&cat=s
- ↑ Canadian Hot 100
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-15. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
- ↑ Swedish Singles chart
- ↑ Billboard Hot 100
- ↑ "Hot R&B/Hip-Hop Singles Sales". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2008-12-05.
- ↑ "Billboard Pop 100". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2008-12-05.
Viungo vya nje
hariri- "Just Stand Up!" katika All Music Guide