Keyshia Miesha Cole (amezaliwa tar. 15 Oktoba 1981)[2] ni msanii wa rekodi za muziki kutoka nchini Marekani. Ametoa albamu yake ya kwanza yenye platinum The Way It Is mnamo Juni 2005, na albamu yake aliyoitoa akiwa chuoni kwa mwaka wa pili iliyoitwa Just Like You hapo mwezi wa Septemba 2007. Albamu yake ya tatu, A Different Me ilitolewa mnamo tar. 16 Desemba 2008, nayo pia imetunukiwa platinum. Pia anajulikana kwa mfululizo wa makala ya tv Keyshia Cole: The Way It Is ambao inarushwa na TV ya BET kuanzia 2006 hadi 2008, kipindi ambacho kinaonesha uhusiano wa Keyshia kikazi na wazazi wake na ndugu pia.

Keyshia Cole

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Keyshia Michelle Cole[1]
Pia anajulikana kama KC, The Princess of Hip-Hop Soul
Amezaliwa 15 Oktoba 1981 (1981-10-15) (umri 42)
Aina ya muziki R&B, hip-hop soul
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi wa nyimbo
Ala Sauti
Aina ya sauti Soprano[2]
Miaka ya kazi 2004–hadi sasa
Studio A&M, Geffen
Ame/Wameshirikiana na Ron Fair, Manny Haley, Remy Ma, Monica, Daniel Gibson, Kanye West, Trina
Tovuti www.keyshiacole.com

Maisha ya awali hariri

Keyshia Cole alizaliwa mnamo tar. 15 Oktoba 1981 mjini Oakland, California, ambapo pia alikulia. Cole alizaliwa na Francine "Frankie" Lons na Sal ambaye ni marehe baba'ke. Baadaye akajakulelewa na Yvonne Cole na familia yake, marafiki wa Frankie, ambao ndiyo waliomlea. Akiwa pamoja na kaka Sean, Keyshia alianza kujionesha kwenye tasnia ya muziki tangu yungali na miaka 12, alikutana na kurekodi na MC Hammer.[3] Baadaye akaanzisha bendi na Tupac Shakur, ambaye alimwahidi kumsaidia kuanzisha kazi zake za uimbaji kabla hajafa kwa kutotarajia.[4] Baada ya kusimamisha uhusiano wake wa zahama, Cole akahamia mjini Los Angeles akiwa na umri wa miaka 18 akiwa na nia ya kujiendeleza zaidi kimuziki. Mwaka wa 2004, baada ya kutoka mixtape, alivutiwa sana na mtendaji mkuu wa A&M Records, Ron Fair,[5] ambaye aliingia naye mkataba na baadaye kuwa mshauri mkuu wake.

Shughuli hariri

2001-2005: Kabla ya The Way It Is hariri

Kabla hajaingia mkataba, Keyshia ameshirikiana na wasanii wale ambao wamezaliwa katika eneo moja la Bay Area, miongoni mwao ni D'Wayne Wiggins wa Tony Toni Tone na Messy Marv.

Katika matarajio yake ya albamu ya kwanza, Keyshia na DJ Green Lantern wakatoa mixtape, Team Invasion Presents Keyshia Cole, kunako mwezi wa Juni 2005. Imeshirikisha muuzo wa sura kama vile Shyne, Remy Ma, Fat Joe na Ghostface Killah. Mixtape imechukua biti ya nyimbo nyingi zilizorekodiwa na wasanii maarufu wa hip-hop kama vile 2Pac ("I Get Around"), Nas' ("Ether"), Mobb Deep ("Shook Ones (Part II)") na Scarface ("Guess Who's Back"). Vibao kama vile cha "(I Just Want It) To Be Over", ambayo ni remix ya "I Changed My Mind", na "I Should Have Cheated" navyo pia viliingizwa.

2004–2005: The Way It Is hariri

Single ya kwanza ya Keyshia ni "Never", ameshirikiana na Eve, ilitolewa mnamo tar. 23 Machi 2004 ili kusukuma kibwagizo cha filamu ya Barbershop 2: Back in Business. Single hii ilianguka kabisa kwenye chati, na Keyshia aliendelea kurekodi albamu yake ya kwanza kwa mwaka mzima wa 2004 hadi mwanzoni mwa mwaka wa 2005. "Never" hatimaye ikawa nyimbo ya mwisho kwenye orodha ya nyimbo za The Way It Is.

Mnamo tar. 9 Novemba 2004, Keyshia ametoa single ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "I Changed My Mind", akishirikiana na Kanye West. Single nafasi ya #71 nchini Marekani, na hakikuwa kibao kikali sana kwa Cole. Single ya pili kutoka katika albamu ni "(I Just Want It) To Be Over", ilitolewa mnamo tar. 5 Aprili 2005, na kufikia nafasi ya #1 kwenye chati Billboard Bubbling Under Hot 100 (#101).

Diskografia hariri

Filmografia hariri

Televisheni hariri

Mwaka Jina
2005 All of Us (Mgeni Mwalikwa)
2006–2008 Keyshia Cole: The Way It Is
2008–2010 Snoop Dogg's Father Hood (Mgeni Mwalikwa)
Paris Hilton's My New BFF (Mgeni Mwalikwa)
BET's 106 and Park (Mgeni Mwalikwa)
BET Awards

Filamu hariri

Marejeo hariri

  1. Joyner, Joyner. Radio Host Knows Who Keyshia Coles father is. Telewatcher. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-08-31. Iliwekwa mnamo 2009-09-07.
  2. 2.0 2.1 Birchmeier, Jason. Keyshia Cole Biography. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-11-02.
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-10-20. Iliwekwa mnamo 2010-10-11.
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-26. Iliwekwa mnamo 2010-10-11.
  5. Keyshia Cole Profile – Biography

Viungo vya Nje hariri