Kadi za adhabu hutumika katika michezo mingi sana: ni aina ya onyo, karipio au kutoa adhabu kwa mchezaji, kocha au afisa wa timu. Kadi za adhabu hutumiwa hasahasa na refa au mwendesha mchezo, na Huonyeshwa endapo mchezaji kafanya kosa. Refa hunyoosha kadi juu huku akimuangalia au akimnyoshea kidole mchezaji aliyefanya kosa. Kitendo hicho ni kwa kusudi la kuonyesha wazi wachezaji wengine pamoja na watazamaji kwamba mchezaji fulani kapewa adhabu fulani. Rangi na umbo la kadi huelezea kiwango cha kosa, vilevile kiwango cha adhabu kwa mchezaji husika. Kadi zinazotumika sana ni kadi ya njano na kadi nyekundu.

Kadi nyekundu wakati wa mchezo wa mpira wa mikono
Kadi ya njano ikitumika katika soka.

Historia na asili

hariri

Wazo la kutumia lugha isiyo na upande ya kadi za rangi kama njia ya mawasiliano baina ya wachezaji na refa ulianza katika mchezo wa soka, refa wa Uingereza Ken Aston ndiye aliyetoa wazo hilo.[1] Bwana Aston aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya FIFA na alikuWa msimamizi wa marefa wote katika fainali za kombe la dunia za mwaka 1966. Katika hatua ya robo fainali timu ya taifa ya uingereza ilikutana na timu ya taifa ya Argentina katika uwanja wa Wembley. Baada ya mchezo huo, magazeti yaliandika habari zinazohusu refa wa mchezo Rudolf Kreitlein kuwapa onyo wachezaji wa Uingereza Bobby Charlton na Jack Charlton, vilevile kumtoa nje mchezaji wa Argentina Antonio Rattín. Refa hakuweka wazi maamuzi yake wakati wa mchezo, baadaye kocha wa Uingereza Alf Ramsey alienda kwa Mwakilishi wa FIFA kupata ufafanuzi zaidi. Tukio hilo lilimfanya Aston afikirie njia mbadala zitakazotumika na refa ili kueleza maamuzi yake kwa wachezaji na watazamaji kwa urahisi zaidi. Aston alibaini kwamba matumizi ya rangi hufuata taratibu zinazofanana (kama tu zile zinazotumika katika taa za barabarani njano – simama kama ni salama, nyekundu – simama) na huvunja vikwazo vya lugha na ingeelezea vizuri kama mchezaji kapewa onyo au kaondolewa kabisa uwanjani.[1]

Matokeo yake, kadi ya njano ilimaanisha mchezaji kapewa onyo na kadi nyekundu mchezaji katolewa nje ya uwanja kabisa na hii ilianza kutumika katika fainali za kombe la dunia mwaka 1970 nchini Mexico. Kuanzia wakati huo, matumizi ya kadi yamekua kwa kasi na kila mchezo ukiongeza sheria zake na kuongeza aina za kadi katika michezo husika.

Aina ya kadi za adhabu

hariri

Kadi ya njano

hariri
 
kadi ya njano hutumika katika michezo mingi na huashiria onyo, au kutolewa nje ya mchezo kwa muda

Kadi ya njano hutumika katika sharia za ishara ya michezo mingi tofauti. Tafsiri yake hotafautiana baina ya michezo; hata na hivyo, kwa kawaida huashiria onyo kwa mchezaji kutokana na tendo Fulani, au huweza kumaanisha kutolewa nje ya mchezo kwa muda mfupi. Mifano hujumuisha:

  • Soka: kadi ya njano huonyeshwa na Refa kuashiria mchezaji Fulani kapewa onyo.[2] Taarifa za mchezaji aliyeonyeshwa kadi huandikwa na refa katika daftari dogo analotembea nalo wakati wote wa mchezo. Mchezaji aliyeonyeshwa kadi ya njano anaweza kuendelea na mchezo; vinginevyo, mchezaji akionyeshwa kadi ya njano kwa mara ya pili, hufuata na kadi nyekundu, maana yake ni mchezaji huyo hataweza kuendelea na mchezo huo tena. Nafasi inayoachwa wazi kwa mchezaji kutolewa nje ya uwanja haiwezi kuzibwa kwa kuingiza mchezaji mwingine ndani. Sheria namba 12 ya sharia za soka zilizoundwa na bodi ya kimataifa ya mpira wa soka na kutumiwa na FIFA) huelezea aina za makossa yanayoweza kupelekea kuonyeshwa kadi ya njano.[2]
     
    Cristiano Ronaldo akionyeshwa kadi ya njano
katika mashindano mengi, mchezaji akionyeshwa kadi ya za njano mfululizo katika mechi tofauti, hupelekea mchezaji huyo kukosa idadi ya michezo kadhaa inayofuata.
  • Riadha katika riadha, kadi ya njano ni ishara ya onyo kwa mchezaji binafsi ikitafsiriwa kwamba enddapo mhezaji huyo ataonyeshwa kai ya njano kwa mara ya pili, itapelekea kuondolewa katika shindano hilo.[3] Sheria za riadha zinazosimamiwa na IAAF zilifuta onyo la kuanza kabla ya kuruhusiwa, kwa sasa kitendo hicho hupelekea kuondolewa kwenye shindano moja kwa moja, kuna mashindano yanayoruhusu onyo, hii huonyeshwa kwa kuonyeshwa kadi yenye rangi za njano na nyeusi.[4] Hata na hivyo, kuanzia mwaka 2012, sheria inayosimamia kudanganya wakati wa kuanza ilibadilika, kwa sasa lazima mikono ya mchezaji itoke kugusa chini au miguu itoke katika viunzi vya kuanzia kabla ishara ya kuanza shindao haijatolewa.

Kadi nyekundu

hariri
 
kadi nyekundu hutumika katika michezo mingi na huashiria kitendo kisicho cha kimchezo na husababisha mchezaji kuondolewa nje ya mchezo na pia kukosa mchezo unaofuata.

kadi nyekundu hutumiwa kama ligha ya ishara katika michezo mingi. Tafsiri yake hutofautiana baina ya michezo, lakini kwa kawaida huonyesha kitendo kibaya kisicho cha kimchezo na mchezaji aliyetenda kitendo hicho hutolewa nje ya uwanja. Katika michezo mingi, mchezaji akitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu, nafasi atakayoiacha uwanjani haitaweza kuzibwa kwa kuingiza mchezaji mwingine. Mifano huumuisha:

  • Soka: kadi nyekundu huonyeshwa na Refa kuashiria mchezaji katolewa nje ya uwanja.[2] Mchezaji aliyeonyeshwa kadi nyekundu atalazimika kutoka nje ya uwanja mara moja na hatoruhusiwa kushiriki katika mchezo huo tena. Mchezaji akitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu, nafasi yake haiwezi kuzibwa kwa kumungiza mchezaji mwingine, na timu yake itawalazimu kuendela na mchezo wakiwa pungufu. Endapo golikipa ataonyeshwa kadi nyekundu, timu inaruhusiwa kumuweka mchezaji wa ndani kuwa golikipa, au kumbadilisha mchezaji wa ndani na golikipa. Kadi nyekundu huonyeshwa kwa mchezaji aliyetenda kosa kubwa mfano kuzuia kwa makusudi mpira usiingie golini kwa njia isiyoruhusiwa. Kadi nyekundu inaweza kuonyeshwa kwa mchezaji endapo ataonyeshwa kadi za njano mara mbili.

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 "Ken Aston – the inventor of yellow and red cards". fifa.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-30. Iliwekwa mnamo Februari 20, 2013. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Laws of the Game". fifa.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-01. Iliwekwa mnamo Juni 6, 2008. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "IAAF Starting Guidelines" (PDF).
  4. "IAAF sanctions immediate disqualification for false starts come January", The Daily Telegraph, August 12, 2009. Retrieved on August 25, 2015. 
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kadi ya adhabu kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.