Cristiano Ronaldo

Mchezaji mpira wa Ureno (aliyezaliwa 1985)

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro,[1][2] GOIH, ComM (matamshi ya Kireno: [kɾiʃ'tjɐnu ʁunaɫdu]; alizaliwa kwenye kisiwa cha Madeira, Ureno, 5 Februari 1985) ni mchezaji soka wa Ureno. Nafasi yake ni mshambuliaji; kwa sasa anacheza nchini Saudi Arabia katika klabu ya Al-Nassr na timu ya taifa lake.

Ronaldo katika kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Ureno
Ronaldo katika kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Ureno

Mara nyingi huchukuliwa kuwa mchezaji bora duniani na kuonekana kuwa mmojawapo kati ya wachezaji wazuri wa nyakati zote. Ronaldo amepata tuzo tano za FIFA Ballon d'Or, ambayo ni zaidi ya mchezaji yeyote wa bara Ulaya, na ni mchezaji wa kwanza katika historia kushinda mara nne viatu vya dhahabu.

Ameshinda tuzo 27 katika kazi yake, ikiwa ni pamoja na mataji matano ya ligi kuu, vikombe vya UEFA Champions League na moja ya UEFA nations league.

Ronaldo[3] atastaafu na kumbukumbu za mabao mengi rasmi yaliyofungwa katika ligi za juu za Ulaya, Ligi ya Mabingwa ya UEFA kwa ngazi ya klabu na ya mataifa, pamoja na magoli mengi yaliyofungwa katika michuano ya UEFA Msimu wa Ligi. Amefunga mabao zaidi ya 600 katika klabu yake na nchi yake.

Maisha

Alizaliwa São Pedro, Funchal, na alikulia parokia ya Funchal ya Santo António, kama mtoto mdogo zaidi wa Maria Dolores dos Santos Aveiro ambaye alikuwa mpishi, na José Dinis Aveiro, aliye kuwa anafanya kazi katika bustani ya manispaa ambaye alikuwa katika kitengo cha muda. Jina la pili alilopewa, "Ronaldo", ni la rais wa Marekani Ronald Reagan. Kaka yake wa kwanza anaitwa Hugo, baada ya kaka yake ana dada wawili, Elma na Liliana Cátia.

Bibi upande wa baba yake anaitwa, Isabel da Piedade, alikuwa anaishi São Vicente, Cape Verde. Ronaldo alikulia katika nyumba ya Wakatoliki maskini, akikaa chumba kimoja na dada yake na kaka yake. Alipokuwa mtoto, Ronaldo alicheza timu ya amateur Andorinha kutoka mwaka 1992 hadi 1995, ambapo baba yake alikuwa mlinzi, na baadaye alitumia miaka miwili kuchezea Nacional.

Mwaka 1997, akiwa na umri wa miaka 12, alijaribu alicheza katika timu ya Sporting CP, alisajiliwa kwa ada ya £ 1,500. Baadaye alihama Madeira kwa Alcochete, karibu na Lisbon, kujiunga na wachezaji wengine wa vijana wa Sporting katika klabu hio.

Akiwa na umri wa miaka 14, Ronaldo aliamini kuwa ana uwezo wa kucheza ligi ya vijana chipukizi, na alikubaliana na mama yake kusitisha elimu yake ili kuzingatia kikamilifu soka. Alipokuwa shuleni na wanafunzi wenzake alimtukana mwalimu na alifukuzwa shule na huyo mwalimu, ambaye alisema "hakumheshimu."

Hata hivyo, mwaka mmoja baadaye, akiwa na umri wa miaka 15, aligunduliwa ana ugonjwa wa moyo, hali ambayo inaweza kumlazimisha kuacha kucheza mpira wa miguu. Alipata upasuaji ambao uliondoa sehemu ya moyo iliyoharibika; alikaa masaa machache hospitali na kurudi nyumbani, alianza tena mafunzo ya mpira wa miguu miezi michache baadaye katika klabu ya Sporting CP, kabla ya kusaini kwa Manchester United akiwa na miaka 18 ndani ya mwaka 2003.

Baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza, Kombe la FA, wakati wa msimu wa kwanza huko Uingereza, alisaidia Machester United kushinda makombe ya ligi kuu ya UEFA Champions League, na Kombe la Dunia la FIFA Club. Alipokuwa na umri wa miaka 22, alikuwa amepokea Ballon d'Or na uteuzi mchezaji bora wa mwaka wa FIFA alipo kuwa na umri wa miaka 23, alishinda mpira wake wa kwanza wa Ballon d'Or na tuzo ya FIFA World ya Mwaka.

Mnamo mwaka 2009, Ronaldo alikuwa mchezaji aliye tumia gharama zaidi kutoka Manchester United kwenda Real Madrid kwa uhamisho wa thamani ya pauni milioni 80.

Katika Hispania, Ronaldo ameshinda tuzo 13, ikiwa ni pamoja na mataji mawili ya La Liga,mataji mawili ya Copa del Rey,mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na michuano mawili ya UEFA Super. Baada ya kujiunga na Real Madrid, Ronaldo alimaliza mchezaji wa Ballon d'Or mara tatu, nyuma ya Lionel Messi, mpinzani wake wa kazi, kabla ya kushinda Ballons d'Or ya 2013 na 2014.

Amepata rekodi 32 ya kufunga bao tatu kwa mpigo ligi ya La Liga, ikiwa ni pamoja na rekodi ya kuunganisha safu nane za bao tatu kwa mpigo katika msimu wa 2014-15 na ni mchezaji pekee wa kufikia magoli 30 ya ligi katika msimu sita wa mfululizo wa La Liga. Mwaka 2014, Ronaldo akawa mchezaji wa kwanza zaidi katika historia kufikia magori 200 ya La Liga, ambayoaliyapa katika mechi 178. Mwaka 2015, na kuifanya klabu yake kuwa na magori mengi zaidi.

Mnamo mwaka wa 2016, Ronaldo alishinda mpira wake wa nne wa Ballon d'Or kwa alama ya kupiga kura baada ya kuifunga La Undécima, nakushika nafasi ya 11 Ulaya, na kushinda Euro 2016.

Ronaldo alikuwa Mchezaji bora zaidi wa Kireno wakati wote wa Shirikisho la Soka la Ureno mwaka 2015. Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwezi Agosti mwaka 2003, akiwa mwenye umri wa miaka 18.

Yeye ni mchezaji aliye shinda zaidi nchini Ureno na na kupata mao tatu kwa mpigo zaidi ya 140, na amehusika katika mashindano makuu saba ambayo yanajumuisha vikombe vitatu vya fifa (2006, 2010 na 2014). Yeye ni mshambuliaji wa juu kabisa Ureno wakati wote. Alifunga bao lake la kwanza la kimataifa mwaka wa Euro 2004 na alisaidia Ureno kufikia fainali. Alikuwa nahodha kamili Julai 2008, akiongoza Ureno kwa ushindi wao wa kwanza katika mashindano makubwa kwa kushinda Euro 2016, na akapokea Silver Boot kama mchezaji wa pili katika mashindano hayo. alikuwa na mchezaji wa kibiashara, alikuwa alikuwa akilipwa zaidi duniani kwa Forbes mwaka 2016 na 2017, pamoja na mwanariadha maarufu zaidi wa dunia na ESPN mwaka 2016 na 2017.

Baada ya wiki moja ya uhamisho tarehe 10 Julai 2018, Ronaldo alisaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Italia iitwayo Juventus baada ya kukamilisha uhamisho wa 100,000,000.

Uhamisho huo ulikuwa wa juu zaidi kwa mchezaji aliyo zaidi ya miaka 30, na ni mchezaji anyaongoza kulipwa na klabu ya Italia hiyo Juventus. Baada ya kusaini, Ronaldo alitoa haja yake na changamoto mpya kama sababu yake ya kuondoka Real Madrid.

Nje ya mpira wa miguu

Kwa kuwa sifa yake ilikua tangu alipokuwa Manchester United[4], Ronaldo amesajili mikataba mingi ya udhamini kwa bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifaa vya michezo , vinywaji, mafuta ya magari, huduma za kifedha, umeme na michezo ya video ya kompyuta (FIFA 18, Pro Evolution Soccer: 2008, 2012, 2013, 2014, 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020.

Tanbihi

  1. "Cristiano Ronaldo vs Lionel Messi: Who is the GOAT in football? The stats head-to-head showdown | Goal.com". www.goal.com. Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
  2. Gill Clark. "Cristiano Ronaldo: 'I'm the Best Player in History,' 'Have Always Thought That'". Bleacher Report (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
  3. "CR7 - Cristiano Ronaldo's Official Website". CR7. Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
  4. "Alejandro Garnacho was perfectly positioned for Cristiano Ronaldo's goal celebration". United In Focus (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2022-05-03. Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cristiano Ronaldo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.