Mto Kagera

(Elekezwa kutoka Kagera, Mto)

Mto Kagera (kwa Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto Nile, pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.

Kagera kwenye maporomoko ya Rusumo. Mto ni mpaka, Tanzania upande wa kushoto na Rwanda upande wa kulia. Vituo vya mpakani vinaonekana darajani.
Ramani ya Mto Kagera.

Unaanzia Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela km 400 hadi kuingia ziwa Viktoria.

Mto Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale unapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho ya njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza km kama 40 kaskazini kwa Bukoba.

Jina la mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Kagera kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.