Karansi
Karansi ni kata ya Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania yenye msimbo wa posta 25403 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,816 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,394 [3] walioishi humo.
Kata ya Karansi imeundwa na vijiji sita vya Karansi, Kandanshi, Lekrimuni, Asheengai, Mendai na Ndinyika. Karansi imekaliwa zaidi na makabila ya Wamaasai, Waarusha, Wachaga, Wameru, na idadi ya makabila mengine ni ndogo sana.
Watu wa Karansi wanajishulisha sana na kilimo, biashara ndogondogo zinazochangiwa kwa uwepo wa soko la Karansi. Pia, huduma za kijamii kama shule, maktaba ya jamii, nyumba za kuabudia, hospitali, barabara zinapatikana kwenye kata hiyo na zimeunganisha vijiji vyote vya kata.
Marejeo
hariri- ↑ [1] Ilihifadhiwa 27 Septemba 2020 kwenye Wayback Machine.Tanzania postcode list, Kilimanjaro region (iliangaliwa Oktoba 2020)
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Siha DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-23.
Kata za Wilaya ya Siha - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||
---|---|---|
Biriri | Donyomurwak | Gararagua | Ivaeny | Karansi | Kashashi | Kirua | Livishi | Makiwaru | Miti Mirefu | Nasai | Ndumeti | Ngarenairobi | Olkolili | Ormelili | Sanya Juu | Songu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Karansi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|