Kasiani wa Imola (alifariki Forum Cornelii, leo Imola, Italia, karne ya 4) alikuwa mwalimu huko Imola, leo katika mkoa wa Emilia-Romagna huko Italia kaskazini) aliyekuwa akifundisha pia imani ya Kikristo.

Kifodini cha Mt. Kasiani, mchoro wa Innocenzo Francucci, 1500 hivi.
Kanisa kuu la Imola (Italia) lina jina lake.

Aliposhtakiwa alikataa kukana imani hiyo ili kuabudu miungu, akaadhibiwa kwa kumfanya auawe na wanafunzi wake kwa kalamu zao [1][2]; hivyo, kadiri mkono ulivyokuwa dhaifu, mateso yalikuwa makali zaidi.

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Agosti[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.