Kassambya
Kassambya ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35314 [1]. Ndani ya kata hii ndimo yalipo makao makuu ya wilaya. [2]
Kata ya Kassambya | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Kagera |
Wilaya | Wilaya ya Misenyi |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 37,028 |
Kaskazini na Magharibi kata hiyo imepakana na kata ya Nsunga, Mashariki imepakana na kata ya Minziro, Kusini imepekana na kata ya Kyaka katika mto Kagera.
Inaundwa na vijiji saba ambavyo ni: Kassambya, Bunazi, Mabuye, Nyabihanga, Gabulanga, Omundongo na Kakindo.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 37,028 [3]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 26,633 waishio humo.[4] Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,933 waishio humo. [5]
Kata hiyo ina shule za sekondari mbili ambazo ni: Shule ya sekondari Bunazi na Shule ya sekondari Gabulanga.
Aidha, kata inazo shule za msingi kumi ambazo ni: Nyabihanga, Omundongo, Bunazi A, Bunazi B, Kabwela, Kassambya, Mature, Itara, Gabulanga na Kakindo.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Jamaldin, Sadam (2024-08-10). "Impact of Banana Production on Smallholder Farmers' Livelihoods in Missenyi District, Tanzania". NG Journal of Social Development. 14 (1): 62–78. doi:10.4314/ngjsd.v14i1.5. ISSN 2814-1105.
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 177
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
- ↑ "Ripoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-12-17.
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kassambya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |