Wilaya ya Missenyi

Wilaya ya Misenyi ni kati ya wilaya za Mkoa wa Kagera, yenye postikodi namba 35300 [1]. Ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Bukoba Vijijini.

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 202,632 [2]

Eneo

Wilaya hii imepakana na Uganda upande wa kaskazini, Ziwa Viktoria upande wa mashariki na Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera upande wa kusini. Eneo la wilaya liko upande wa magharibi ya Ziwa Viktoria.

Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi (Missenyi District Council) ni moja kati ya serikali 8 za kiwilaya kwenye Mkoa wa Kagera. Eneo la wilaya ni km² 2709.

Tabianchi

Maeneo ya wilaya hupokea mvua mara mbili kwa mwaka; kwenye mwambao wa Ziwa Viktoria mvua hufikia hadi milimita 1,400 na 2,000 kwa mwaka, kwenye nyanda za juu kati ya mm 1,000 na 1,400; upande wa magharibi kiwango hushuka hadi mm 600 na 1,000 kwa mwaka.

Usafiri

Barabara ya lami T4 kutoka Mwanza inapita Missenyi ikielekea Uganda. Barabara ya vumbi T38 inaanza kwenye T4 pale Kyaka ikielekea Wilaya ya Ngara, kupitia Wilaya ya Karagwe.[3]

Marejeo

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
  3. Kagera Roads Network. Jalada kutoka ya awali juu ya 23 February 2016. Iliwekwa mnamo 16 February 2016.

Viungo vya Nje

  Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania  

Bugika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Missenyi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.