Bugorora ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35311 [1].

Kata ya Bugorora
Nchi Tanzania
Mkoa Kagera
Wilaya Wilaya ya Missenyi
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 8,105

Mto Kagera na mto Ngono inapita katika kata hiyo.

Kata ina vijiji vitatu ambavyo ni Bugorora, Buchulago na Kabingo. Kijiji cha Bugorora ndiyo kimebeba jina la kata hiyo na ndipo yalipo makao makuu ya kata.

Kijiji cha Bugorora kina vitongoji kama Kagarama, Bugorora A (Mitaro), Bugorora B (Omukibindo), Mibalayangwe, Kagezi, Rukindo na Nkenge.

Kijiji cha Kabingo kina vitongoji kama Ngorogoro, Kyabugombe, Kabingo Igoma na Kashenye.

Kijiji cha Buchurago kina vitongoji kama Kamwisa, Iyorohoro, Mabale.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 8,105 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,905 waishio humo.[3]

Kata ya Bugorora ina shule ya sekondari moja inayoitwa Nkenge ambayo inachukua jina la jimbo la Nkenge.

Pia ina shule za msingi 4 ambazo ni Bugorora Ps, Gwankimba Ps, Kyabugombe Ps na Buchurago Ps.

Soko la kata hiyo ni kila Jumanne Bugorora mjini.

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 177
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
  Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania  

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bugorora kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.