Nsunga
Nsunga ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35316 [1].
Baadhi ya vijiji katika kata hiyo ni pamoja na:
- Igayaza
- Ngando
- Omurugando
- Byamutemba
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 26,772 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,001 waishio humo.[3]
Nsunga ni kata inayokua kwa kasi, na uchumi wake unaotegemea kilimo unakwamua watu wengi katika umaskini. Watu wanaoishi katika kata hiyo wanajihusisha na kilimo cha kahawa, ndizi, mboga, na ufugaji. Ni kata ambamo ndani yake kuna kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar, hivyo wakazi hujihusisha na kilimo cha miwa pia.
Kata hiyo imekuwa na umaarufu kwa kuwa na ukanda wenye kutuama maji, ambapo nyakati za kiangazi hutumika katika kuzalisha mboga za majani na matunda. Maeneo haya ni pamoja na Kyarukorongo, Kigwanga na Gelegele, ambako mboga nyingi huzalishwa. Wakulima hao hutegemea soko kuu la Bunazi, lililoko wilaya ya Missenyi.
Historia
haririKata hiyo ina milima mingi ambayo ilitumika zaidi katika vita vya Kagera (1978-1979).
Tarehe 10 Septemba 2016 Nsunga ilikuwa mahali pa kitovu cha tetemeko la ardhi la Kagera 2016.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 177
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nsunga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |