Kassim Bizimana

Kassim Bizimana (amezaliwa katika mji wa Bujumbura 29 Desemba 1985) ni mchezaji wa mpira wa miguu, hasa mshambuliaji, kutoka nchi ya Burundi.

Kassim Bizimana
Kassim bizimana-1541349976.jpg
Maelezo binafsi
Jina kamili Kassim Bizimana
Tarehe ya kuzaliwa 29 Desemba 1985 (1985-12-29) (umri 34)
Mahala pa kuzaliwa    Bujumbura, Burundi
Nafasi anayochezea Mshambuliaji
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa VV Gieten
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2005 BV Veendam
Timu ya taifa
2008 Burundi

* Magoli alioshinda

Anaichezea klabu ya BV Veendam katika ligi ya pili Uholanzi (kwa Kiholanzi Eerste Divisie).

Aliichezea nchi yake ya Burundi katika mechi za kimataifa. Mwaka wa 2007 timu ya taifa ya Rwanda ilijaribu kumuomba achezee timu yao, lakini mchezaji huyo alichagua kuichezea timu ya Burundi.

Kassim Bizimana ana pasipoti ya Uholanzi na hiyo ni kutokana na muda mrefu ambao ameishi huko Uholanzi.

Kucheza kwake UlayaEdit

Bizimana alichezea klabu za vijana za SC Heerenveen na Achilles 1894. Alianza kuwa mchezaji wa kulipwa mwaka 2004 kwenye klabu ya FC Groningen. Mechi yake ya kwanza kabisa na klabu yake hiyo ilikuwa tarehe 22 Oktoba 2004 dhidi ya Willem II Tilburg pindi alipomgomboa mchezaji (Jack Tuyp) katika dakika ya 74. Groningen ilifungwa 4-2.

Katika Julai 2005, aliuzishwa katika klabu ya BV Veendan. Bizimana alionekana kuwa mchezaji mzuri na anashiriki dakika nyingi na timu yake hiyo na ni kiungo muhimu sana katika klabu yake hiyo na kwa sasa ndio timu anayoichezea.

Bizimana ana mechi 13 katika timu yake ya taifa ya Burundi na ana magoli manne.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kassim Bizimana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.