Cherero

Ndege wadogo kiasi wa familia Psittaculidae
(Elekezwa kutoka Kasuku-mapenzi)
Cherero
Cherero kichwa-machungwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Psittaciformes (Ndege kama kasuku)
Familia: Psittaculidae (Ndege walio na mnasaba na kasuku wadogo)

} bingwa_wa_familia = Vigors, 1825

Jenasi: Agapornis
Selby, 1836
Ngazi za chini

Spishi 9:

Cherero au kasuku-mapenzi ni ndege wa jenasi Agapornis katika familia Psittaculidae. Ndege hawa ni aina ya kasuku wadogo na wana rangi kali. Mkia wao ni mfupi kuliko kasuku wengine lakini kama hawa miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Cherero wanatokea Afrika na Madagaska. Hula matunda, mboga, mbegu na pengine wadudu. Dume na jike wanaishi pamoja kwa maisha yao yote. Hupitisha muda mrefu wakikaa karibu sana. Kwa hivyo huitwa kasuku-mapenzi pia. Jike huyataga mayai 3-8 tunduni kwa mti.

Spishi

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cherero kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.