9 Novemba
tarehe
Okt - Novemba - Des | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 9 Novemba ni siku ya 313 ya mwaka (ya 314 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 52.
Matukio
hariri- 694 - Egica, mfalme wa Wavisigothi wa Hispania, anawashutumu Wayahudi kuwasaidia Waislamu, na anawaadhibu kuwa watumwa
- 1282 - Papa Martin IV anamtenga na Kanisa mfalme Petro III wa Aragona
- 1494 - Akina Medici wanaanza kutawala mji wa Florence
- 1799 - Napoleon Bonaparte anapindua serikali ya Ufaransa.
- 1848 - Robert Blum anauawa katika mji wa Vienna
- 1872 - Moto unateketeza sehemu kubwa ya mji wa Boston
- 1918 - Kaizari Wilhelm II wa Ujerumani anajiuzulu, na Ujerumani unatangazwa kuwa jamhuri
- 1938 - Usiku wa Chembechembe (kwa Kijerumani: Reichskristallnacht), ambapo WaNazi wanatumia nguvu na vurugu dhidi ya Wayahudi
- 1989 - Nchi ya Ujerumani wa Mashariki inafungulia Ukuta wa Berlin na kuwaruhusu wananchi wake kusafiri bila shida kwenda Ujerumani wa Magharibi
Waliozaliwa
hariri- 1897 - Ronald Norrish, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1967
- 1918 - Spiro Agnew, Kaimu Rais wa Marekani
- 1923 - James Schuyler, mshairi kutoka Marekani
- 1928 - Anne Sexton, mshairi kutoka Marekani
- 1929 - Imre Kertesz, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 2002
- 1952 - Jack Szostak, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2009
- 1971 - Big Pun, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1988 - Cali Sweets, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
Waliofariki
hariri- 1952 - Chaim Weizmann
- 1982 - Shaykh 'Abdullaah Swaalih Al-Farsy, mwanahistoria kutoka Zanzibar
- 2011 - Har Khorana, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1968
Sikukuu
haririWakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha sikukuu ya Kutabaruku Kanisa Kuu la Roma, lakini pia kumbukumbu za watakatifu Ursino wa Bourges, Agripini wa Napoli, Vito wa Verdun, Eustolia na Sopatra, Joji wa Lodeve, Elizabeti wa Utatu n.k.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 9 Novemba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |