Khalifa bin Harub wa Zanzibar

Sayyid Khalifa II bin Harub Al-Said (* 26 Agosti 1879 - + 9 Oktoba 1860) (kwa maandishi ya Kiarabu خليفة بن حارب البوسعيد) alikuwa mtawala wa 9 wa Usultani wa Zanzibar.

Alikuwa sultani kuanzia 9 Desemba 1911 hadi 9 Oktoba 1960. Hali halisi alikuwa mtawala kwa jina tu wakati mamlaka ya serikali ilikuwa mkononi mwa afisa mkazi Mwingereza.

Mwaka 1900 akamwoa Sayyida Matuka bint Hamud Al-Busaid aliyekuwa binti wa sultani wa saba wa Zanzibar Sayyid Hamud bin Muhammed Al-Busaid.

Aliyemfuata alikuwa mwana wake Abdullah bin Khalifa sultani wa mwisho kisiwani. [1]

Marejeo

hariri
  1. Zanzibar, [1]
Alitanguliwa na
Ali bin Hamud
Sultani wa Zanzibar
1911–1960
Akafuatiwa na
Abdullah bin Khalifa