Muhammad ibn Musa al-Khwarizmi (Kiarabu: محمد بن موسى الخوارزمي; Al-Khwarizmi kwa ufupi) alikuwa mtaalamu wa dola la Waabasiya aliyeishi muda mrefu mjini Baghdad na kuandika kazi za lugha ya Kiarabu zenye ushawishi mkubwa kwenye hisabati, elimuanga na jiografia.

Muhammad ibn Mūsā al-Khwārizmī
Stempu ya Umoja wa Kisovyeti iliyotolewa kwa heshima ya sikukuu ya 1200 ya Kwarizmi
Stempu ya Umoja wa Kisovyeti iliyotolewa kwa heshima ya sikukuu ya 1200 ya Kwarizmi
Alizaliwa mnamo 780 BK
Alikufa mnamo 850
Nchi Dola la Waabasiya
Kazi yake mtaalamu wa hisabati, jiografia na falaki
Sanamu ya mbao ya karne ya 20 ikimsadifu Al-Khwarizmi.

Alizaliwa katika familia ya Kiajemi yenye asili katika kwenye milki ya Khwarezm. Haijulikani kama yeye mwenyewe alizaliwa huko. Hakuna habari alisoma wapi.

Khwarizmi alifanya kazi kwa muda mrefu katika Dar-al-Hikma (nyumba ya hekima) iliyokuwa kama chuo kikuu kilichoundwa na khalifa Harun ar-Rashid.

Katika kitabu chake juu ya "Mahesabu kwa kutumia namba za Kihindi" alionyesha faida ya hisabati ya Kihindi akaeleza namba sifuri. Hivyo aliweka msingi wa hisabati ya kisasa. Vitabu vyake vilitafsiriwa katika lugha mbalimbali vikasambazwa kwa Kilatini pia katika Ulaya.

Ukurasa kutoka kitabu cha Khwarizmi juu ya hisabati

Aliandika pia juu ya jiografia ya Ptolemayo akashiriki katika uchoraji wa ramani ya dunia kwa matumizi ya khalifa.

Utaalamu wake kuhusu falaki alitumia kwa vitabu vyake juu ya kalenda.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khwarizmi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.