Kibosho Mashariki
Kibosho Mashariki ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Msimbo wa posta ni 25216.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,996 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,148 walioishi humo[2].
Wakazi wengi wa kata hii ni Wakatoliki japo kuna waumini wachache wa imani nyingine kama Waislamu, Wapentekoste, Mashahidi wa Yehova n.k. Wamisionari wa kwanza kabisa wa Kiroma kuingia Mkoa wa Kilimanjaro walijenga kanisa kubwa la kihistoria la Kikatoliki ambalo lina umri mkubwa sana Tanzania. Kata ya Kibosho Mashariki ina huduma zote za kijamii kama hospitali kubwa, shule za sekondari shule za msingi pamoja na vyuo mbalimbali. Vyuo vinavyopatikana ni kama Chuo cha Ufundi FDC, Chuo cha Ualimu Singa Chini, Chuo cha Mtakatifu Stefano Moshi na Chuo cha Uuguzi Kibosho.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kibosho Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|