Marangu Magharibi
Marangu Magharibi ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,976 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25222
Marangu Magharibi ina vijiji 7 na watu wake walio wengi ni wafanyabiashara na wengine wameajiriwa kwenye sekta za binafsi na serikali kwa ujumla. Hata hivyo, ni moja kati ya sehemu maarufu sana, na eneo lake lina rutuba nyingi kwa kilimo kidogo cha ardhi ya hapo iliopo. Ardhi ya eneo hili limerithishwa kwa mtililiko wa kifamilia (mfumo wa "Kihamba"). Umaskini katika eneo hili bado umeonekana kuwa tatizo kubwa lakini linashughulikiwa ukifananisha na sehemu nyingine za mabonde ya Mlima Kilimanjaro. Kuna mito kadhaa inayomwagikia hapa na vilevile vyanzo vya maji ya chemchem.
Marejeo hariri
- ↑ Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Marangu Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|