Kilema Kusini
Kilema Kusini ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,711 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25226.
Askofu Mkuu wa Mwanza (tangu mwaka 2011) Juda Thadaeus Ruwa'ichi alizaliwa hapa mwaka 1954 katika kijiji cha Mulo.
Kilema pia ni sehemu inayotukuzika kihistoria kwani mche wa kwanza wa kahawa Tanzania ulioteshwa Kilema. Wenyeji wanaamini kuwa chimbuko la jina la mlima Kilimanjaro pia lilianzia Kilema. Watu walikuwa wakiuita mlima huo Kilema Kyaryo "yaani kilima cha kupanda" lakini wageni wakashindwa kutamka na kusema Kilimanjaro.
Marejeo hariri
- ↑ Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kilema Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|