Kidogo
"Kidogo" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 12 Julai 2016 kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akishirikisha kundi la P-Square kutoka nchini Nigeria.
“Kidogo” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava ya Kidogo
| |||||
Single ya Diamond Platnumz na P-Square kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale | |||||
Imetolewa | 12 Julai, 2016 | ||||
Muundo | Upakuzi wa mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2016 | ||||
Aina | Bongo Flava, Afro-pop | ||||
Urefu | 4:14 | ||||
Studio | Wasafi Records | ||||
Mtunzi | Diamond Platnumz P-Square | ||||
Mtayarishaji | Shirko V-Tek Laizer Classic | ||||
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na P-Square | |||||
|
Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa tatu kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na watayarishaji watatu tofauti kabla kuja kumaliziwa mazima katika studio za Wasafi Records. Ndani yake kuna mkono wa Shirko (katengeneza biti), V-Tek (kaichanganya na kuiboresha zaidi) na mwisho kabisa akamalizia Laizer Classic aliyefanya marekebisho ya mwisho kabisa. Kazi ya kutunga wimbo huu ilianza tangu tarehe 10 Januari 2015 katika studio za Square Records, Lagos Nigeria kabla kuja kutia masauti.<ref>VIDEO: Diamond Platnumz ft. PSquare – Kidogo Naija Vibes - 2016.
Video yake imefanywa jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini chini ya Godfather Productions mnamo tarehe 24 Aprili, 2016. Si muda mrefu hadi kuja kuachiwa. Hii ni video ya sita kufanya pamoja na Godfather tangu Mdogo Mdogo, Ntampata Wapi, Nana], Utanipenda, Make Me Sing na huu.