Nyoka-mchanga

(Elekezwa kutoka Kidurango)
Nyoka-mchanga
Kidurango (Psammophis angolensis)
Kidurango (Psammophis angolensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Psammophiinae (Nyoka walio na mnasaba na nyoka-mchanga)
Dowling, 1967
Jenasi: Psammophis
Fitzinger, 1826
Ngazi za chini

Spishi 34:

Nyoka-mchanga ni spishi za nyoka wa jenasi Psammophis katika familia Lamprophiidae. Nyoka-mchanga mdogo huitwa kidurango pia.

Nyoka hawa ni wafupi hadi warefu kiasi. Spishi nyingi ni sm 50-100 lakini nyoka-mchanga maridadi ni sm 45 kwa kipeo na nyoka-mchanga madoadoa anaweza kufika m 1.9. Kimsingi rangi yao ni kahawia lakini kwa kawaida wana milia myeusi, kijivu, njano na/au myekundu.

Nyoka-mchanga hula mijusi ambao wanawakamata ardhini au katika vichaka.

Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa na ni ndefu kuliko zile za nyoka wengine wenye chonge za nyuma. Spishi kubwa zinaweza kuingiza kiasi cha sumu kinachotosha kwa kumletea mtu shida: kufura, kuvuja damu, unyeo mbaya na kichefuchefu.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-mchanga kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.