Kifutio
Kifutio au raba (kutoka Kiingereza rubber) ni kifaa kinachotumiwa kufuta alama za penseli au aina za kalamu. Kimsingi ni kipande kigumu cha mpira kinachotumiwa kufutia maandishi.
Mara nyingi kipande kidogo cha mpira kimefungwa kwenye penseli yenyewe wakati inapotengenzwa. Ilhali vipande vidogo huisha haraka au kuvunjika ni afadhali kuwa na kipande kikubwa.
Ziko aina tofauti hasa katika kiwango cha ugumu; tofauti nyingine ni uundaji kutokana na utomvu wa mpira au plastiki.
Fizikia ya kifutio - raba
haririPenseli huandika kwa kuweka grafati kwenye uso wa karatasi; vipande vya grafati hushikwa kwa nguvu ya mng'ang'aniano; ule mng'ang'aniano baina ya mpira na grafati una nguvu zaidi kuliko ule baina ya karatasi na grafati. Wakati unaburuza raba juu ya karatasi, uso wake unashikana na grafati. Hapo ni muhimu kwamba raba inaachana na vipande vya uso wake vilivyojaa grafati tayari ili sehemu mpya ya uso wake iwe tayari kupokea vipande vingine vya grafati. Hivyo matumizi ya kifutio yanaacha chembe ndogo kwenye uso wa karatasi ambazo tunaweza kuondoa kirahisi kwa kuzipangusa au kupuliza.
Kifutio cha ubao
haririKuna pia kifutio kinachotumiwa kwenye ubao k.m. shuleni. Hicho huitwa pia dasta (ing. duster). Kwa kawaida ni kipande cha kitambaa au sifongo kinachotumiwa kuondoa alama za chaki kwenye ubao wa shule.
Viungo vya Nje
hariri- Eraser: How Products are Made, Volume 5 (1997) by Rose Secrest
- Pearlstein, Cabelli, King, A. : Effects of Eraser Treatment on Paper, Journal of the American Institute for Conservation 1982, volume 22
- Goodyear Rubber History Archived 2008-05-09 at the Wayback Machine
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |