Penseli (kutoka Kiingereza: pencil) ni kifaa cha kuandikia au kuchorea kinachofanywa na kiini thabiti cha grafati au mata nyingine yenye pigmenti kilichopo ndani ya gamba linalokinga kiini kisivunjike.

Penseli.
Penseli iliyopasuliwa.

Penseli inachora kwa kuacha alama za vipande vidogo vya kiini chake kwenye karatasi au uso mwingine unapokandamizwa juu yake.

Penseli ni tofauti na kalamu zinazotoa wino kwenye karatasi.

Muundo

hariri

Viini vya penseli kwa kawaida hutengenezwa kwa kuchanganya unga wa grafati na unga wa udongo wa mfinyanzi. Penseli za aina hiyo huacha alama nyeusi au za kijivu zinazoweza kufutwa tena lakini zinadumu hata zikiathiriwa na unyevu, maji, kemikali nyingi au mwanga wa Jua.

Siku hizi mchanganyiko wa grafati na udongo wa mfinyanzi hufanywa kiwandani; mchanganyiko huu unatolewa kama nyuzi zenye kipenyo cha milimita chache na kuokwa kwa joto, halafu kufungwa ndani ya gamba la ubao.

Penseli hutengenezwa kwa ugumu tofauti; tofauti hizo huhusika na ugumu au ulaini wa kiini; penseli laini inaruhusu kubadilisha upana wa mstari wa kuchora kwa kuongeza shinikizo au kulipunguza. Penseli laini hupendelewa zaidi na wasanii kwa kuchora. Kinyume chake penseli ngumu hufaa zaidi kwa kuandika.

Historia

hariri
 
Penseli za rangi.

Vifaa vya kufanana kiasi na penseli vilitumiwa tangu kale ambako vijiti vyenye ncha kali vilitumiwa kuchora alama au kuandika kwenye bao za nta au za udongo wa mfinyanzi. Kulikuwa pia na penseli za plumbi ambazo zinachora mistari hafifu.

Mnamo mwaka 1600 hivi akiba ya grafati safi iliyokaa karibu na uso wa ardhi ilitambuliwa Uingereza. Grafati hiyo ilikatwa na kuuzwa kote Ulaya[1]. Baada ya kujulikana kwa faida ya penseli za grafati, na ilhali akiba hiyo ilikuwa ya pekee, michanganyiko ya grafati na udongo ilianza kutumiwa penginepo Ulaya.

Kuna pia penseli za rangi ila tu hapa kiini si tena ya grafati bali ya michanganyiko ya pigmenti pamoja na nta au mafuta mbalimbali.

Tanbihi

hariri
  1. [http://www.cumbria-industries.org.uk/wad/ Wad,a shortened version of the chapter by Dave Bridge in Lakeland’s Mining Heritage] Ilihifadhiwa 13 Mei 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Industrial History of Cumbria, iliangaliwa Desemba 2019

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Petroski, Henry (1990). The Pencil: A History of Design and Circumstance. New York: Alfred A. Knopf. ISBN 978-0-394-57422-6.
  • How A Pencil Is Made katika YouTube
  • Inside one of America's last pencil factories NYTimes, 12 January 2018
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.