Singapuri ni nchi ndogo katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Singapuri
Ramani ya Singapuri

Jiografia hariri

Eneo lake ni kisiwa kwenye ncha ya kusini kabisa ya Rasi ya Malay pamoja na visiwa vidogo vya kando. Kisiwa kimetenganishwa na bara kwa mfereji mwembamba wa Johor.

Kuna mji mmoja tu: ni jiji la Singapuri lilipopo kisiwani, hivyo huhesabiwa pia kati ya dola-miji.

Historia hariri

Kisiwa kiliwahi kuwa na makazi mbalimbali katika historia. Mji wa kisasa ulianzishwa mwaka 1819 na Waingereza kama kituo cha biashara ikawa bandari muhimu ya eneo.

Uingereza uliipa uhuru kama sehemu ya shirikisho la Malaysia. Lakini matatizo ya kuelewana yalionekana haraka kati ya wanasiasa Wamalay wa bara na wenzao Wachina wa kisiwani.

Mwishowe Singapuri ikafukuzwa katika shirikisho ikawa nchi ya kujitegemea tarehe 9 Agosti 1965. Mwanasiasa Lee Kuan Yew alikuwa waziri mkuu wa kwanza akaendelea na cheo hiki hadi mwaka 1990 akaongoza Singapuri kuwa kati ya mataifa matajiri ya Asia.

Wakazi hariri

Kati ya wakazi milioni tano na nusu walio wengi (74.3%) ni wa asili ya China. Mababu wao walihamia huko wakitafuta kazi bandarini.

Wengine ni wakazi asilia Wamalay (13.5%) na Watamil na wengineo waliotokea Uhindi (9%).

Kuna lugha 24 ambazo huzungumzwa nchini Singapuri. Lugha rasmi ni Kiingereza (48.3%), Kichina (38.6%), Kimalay (9.2%) na Kitamil (2,5%).

Upande wa dini, 31.1% ni Wabuddha, 18.9% ni Wakristo, 15.6% ni Waislamu, 8.8% ni Watao, 5% ni Wahindu.

Uchumi hariri

Uchumi wa Singapuri unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda.

Imekuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa Asia ya Kusini.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Biashara
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Singapuri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.