Kipanya matiti-mengi
Kipanya matiti-mengi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya matiti-mengi wa kawaida (Mastomys natalensis)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 8:
|
Vipanya matiti-mengi ni wanyama wagugunaji wa jenasi Mastomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae walio na matiti mengi kuliko panya wote wengine. Wanatokea katika savana, nusu-jangwa na msitu|misitu]] kavu ya Afrika kusini kwa Sahara.
Maelezo
haririWanyama hawa wanafanana na panya wa kawaida (jenasi Rattus) lakini ni wadogo zaidi. Urefu wa mwili ni sm 6-17, urefu wa mkia ni sm 5-15 na uzito ni g 12-70. Manyoya ni mafupi na mororo yenye rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na kijivu au nyeupe tumboni. Majike wana matiti mengi kuliko panya wengine: 10-24 kulingana na spishi.
Wanatokea katika maeneo kavu na hukiakia usiku. Wanalala katika viota vya mimea kavu wanayojenga katika nyufa za miamba, chini ya mizizi ya miti, chini ya miti iliyoanguka au katika vishimo. Hula mbegu, matunda, nyasi na invertebrata wadogo, na pengine nyama mbichi ya mizoga au kutoka nyumba (kipanya matiti-mengi wa kawaida).
Kwa kawaida majike huzaa mikumbo miwili kwa mwaka, pengine 3-4. Kuna wachanga 6-12 kwa mkumbo kwa kawaida, lakini wachanga wanaweza kuwa hadi 22. Mimba huchukua karibu siku 20.
Kipanya matiti-mengi wa kawaida na yule wa kusini (M. natalensis na M. coucha) huishi katika majengo mara nyingi na wanaweza kuwa wasumbufu wabaya. Hata wanaweza kuenea magonjwa, tauni hasa. Yule wa kawaida ni hazina muhimu ya virusi ya Lassa.
Spishi
hariri- Mastomys awashensis (Awash multimammate mouse)
- Mastomys coucha (Southern multimammate mouse)
- Mastomys erythroleucus, Kipanya matiti-mengi magharibi (Guinea multimammate mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda
- Mastomys huberti (Hubert's multimammate mouse)
- Mastomys kollmannspergeri (Verheyen's multimammate mouse)
- Mastomys natalensis, Kipanya matiti-mengi wa kawaida (Natal multimammate mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Mastomys pernanus, Kipanya matiti-mengi mdogo (Dwarf multimammate mouse) – Kenya, Rwanda, Tanzania
- Mastomys shortridgei (Shortridge's multimammate mouse)
Picha
hariri-
Kipanya matiti-mengi kusi
-
Matiti ya kipanya matiti-mengi wa kawaida