Kipanyanyasi-milia

Kipanyanyasi-milia
Kipanyanyasi-milia wa kawaida katika Msitu wa Kakamega (Lemniscomys striatus)
Kipanyanyasi-milia wa kawaida katika Msitu wa Kakamega (Lemniscomys striatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Lemniscomys
Trouessart, 1881
Ngazi za chini

Spishi 11:

Vipanyanyasi-milia ni wanyama wagugunaji wa jenasi Lemniscomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika mbuga za Afrika.

Maelezo

hariri

Panya hawa wana mlia mweusi mgongoni na spishi wengine zina milia na madoa mengine pia. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 95-150 na uzito ni g 18-70.

Kwa ujumla huzingatiwa kukiakia wakati wa mchana, lakini angalau spishi kadhaa zinaweza kukiakia usiku. Hula majani, mizizi na mbegu na mara kwa mara wadudu pia.

Kuna wachanga hadi 12 kwa kila mkumbo, lakini 4-5 ni kawaida zaidi. Wanaweza kuwa na mikumbo minne katika kipindi cha chini ya miezi minne. Wastani wa matarajio ya muda wa kuishi ni mfupi sana, porini mara nyingi mwaka mmoja tu, lakini L. striatus aliishi kwa karibu miaka 5 kifungoni.

Spishi

hariri