Kisangu (lugha ya Tanzania)

Kisangu (au Kisango; pia huitwa Kirori) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasangu.

Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisangu iko katika kundi la G60.

Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kisangu ilihesabiwa kuwa watu 75,000.

Maeneo ya Kisangu hariri

Lugha ya Kisangu tangu miaka ya 1980 imeanza kufifia kutokana na kuwepo kwa mwingiliano wa makabila mengine, hasa ya Wahehe na Wabena, ambao walihamia katika miji ya Rujewa, Ubaruku na baadhi ya maeneo ya kaskazini magharibi mwa wilaya ya Mbarali kwa ajili ya shughuli za kilimo cha mpunga ambacho kimekuwa tegemeo kubwa la wakazi wa wilaya hiyo: hivyo wengi wao wanazungumza lugha ya Kijewa ambayo ni mchanganiko wa lugha za Kihehe, Kibena na Kisangu chenyewe.

Lugha ya Kisangu inazungumzwa ipasavyo katika kata za Utengule Usangu, Msangaji na baadhi ya maeneo ya Kata ya Mapogoro.

Baadhi ya tamaduni zinazoendeshwa katika maeneo ya Rujewa na Ubaruku si tamaduni asilia za kisangu mfano neno la kiswahili, Unasemaje? Kwa Kisangu ni, wijashi? na rugha yakijewa witigira ndauli? Pia lugha ya Kisangu mara nyingi maneno yake huanza na kh. mfano khakhija shi? khakhayinsile, khakhene n.k.

Mbali na kuwepo kwa makabila tajwa hapo juu,pia makabila ya wanyakyusa toka Wilaya ya Rungwe, wandali toka wilaya ya Ileje na Wawanji toka wilaya ya Makete yameendelea kuongezeka kusini magharibi mwa wilaya hiyo ya mbarali hususani katika miji ya Chimala, Igurusi, Mswiswi na maeneo ya kata ya Ilongo ambapo kabila hilo la wasangu limekuwa likiathiliwa sana na makabila hayo kutokana na wengi wa wasangu kutumia lugha hizo katika mazungumzo yao ya kila siku.

Pia idadi ya Wasangu wanaozungumza lugha hiyo katika wilaya ya mbarali imekuwa ikipungua kila mwaka kutokana na sababu kuu mbili,kwanza ni udogo wa idadi ya wasangu katika wilaya hiyo ya Mbarali na idadi ya wasangu waliowengi si wapenzi wa kuzungumza lugha hiyo kama ilivyo kwa makabila mengine mfano ya wasukuma,wanyakyusa na wamasai.

Asilimia 90 ya wakazi wa wilaya ya Mbarali wanajishughurisha na kilimo cha Mpunga hali ambayo imepelekea wilaya hiyo kuwa ya Kwanza nchini Tanzania kwa uzalishaji wa zao la Mpunga,pia wilaya hiyo imekaa kwa mfano wa bwawa kutokana na kuzungukwa na safu za milima ya kipengele na safu za milima ya Chunya ambayo kwa kiasi kikubwa hutililisha maji ya kutosha katika eneo hilo,huku idadi kubwa ya wakazi hao wakilima kilimo bila ya kutumia mbolea.

Hata hivyo lugha hiyo ya kisangu ina mvuto mkubwa wakati wa kuzungumza kutokana na matamshi yake wkati wa kuzungumza, na baadhi ya wageni ambao wameweza kuimudu lugha hiyo wamekuwa wapenzi wakubwa wa kuizunguza.

Marejeo hariri

  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

  • Heese, Paul. 1919/20. Die Sango-Sprache: eine kurze Grammatik für Anfänger. Zeitschrift für Eingeborenen-Sprachen, 10, uk.87-106.

Viungo vya nje hariri