Rujewa ni kata ya Wilaya ya Mbarali katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Kata ya Rujewa
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbarali
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 42,013

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 42,013 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 29,473 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 53601.

Historia ya Rujewa

hariri

Jina Rujewa linatokana na mtu wa kwanza kuishi Rujewa aliyeitwa Mjewa, aliyekuwepo miaka mingi na familia yake wakaitwa Wajewa, ndiyo sababu hata leo hii pakaitwa Rujewa.

Watawala wa jadi

hariri

Wenyeji wa mwanzo Rujewa walikuwa Wasangu waliokuwa na mtawala wao wa jadi aliyeitwa Chifu Merere, lakini pia kuna Wabena, Wakinga na hata kuna Waburushi kutoka Pakistan ambao hufanya shughuli kwa kushirikiana na wenyeji.

Uchumi

hariri

Rujewa iko katika tambarare ya Usangu ambako maji ya mito kutoka milima ya jirani yanakusanyika na kuwa chanzo cha Mto Ruaha Mdogo. Hivyo eneo linatumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji hasa ukiangalia ndiko yaliko mashamba ya Mbarali Estate.

Rujewa ni maarufu hasa kwa kilimo cha mpunga kule Kapunga, ambao unasifika kuwa mzuri kuliko eneo lolote la Tanzania, na baadhi ya mazao ya biashara yanayolimwa Rujewa ni kama alizeti. Pia Rujewa yanastawi mazao mengi ya chakula kama vile karanga, mahindi, ulezi n.k.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbarali DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-14.
  Kata za Wilaya ya MbaraliMkoa wa Mbeya - Tanzania  

Chimala | Igava | Igurusi | Ihahi | Imalilo Songwe | Ipwani | Itamboleo | Kongolo | Lugelele | Luhanga | Madibira | Mahongole | Mapogoro | Mawindi | Miyombweni | Mwatenga | Ruiwa | Rujewa | Ubaruku | Utengule Usangu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rujewa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.