Kitabu cha Hali ya Hewa
Kitabu cha Hali ya Hewa ni kitabu cha pamoja kisicho cha uwongo kilichoongozwa na mwanaharakati wa hali ya hewa Greta Thunberg. Kina mkusanyo wa insha fupi na wataalamu zaidi ya mia moja. Kinachambua sababu, matokeo na changamoto za mgogoro wa hali ya hewa.
Toleo la Kiingereza lilichapishwa mnamo Oktoba 2022. Tafsiri huchapishwa katika lugha kadhaa zikiwemo Kijerumani, Kihispania, Kireno, Kiitalia, Kifaransa, Kiholanzi, Kiswidi, Kideni na Kinorwe.
Jalada lina mchoro wa taswira ya data ya mistari ya joto ya aina iliyotengenezwa na mtaalamu wa hali ya hewa Mwingereza Ed Hawkins.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Hali ya Hewa kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |